Hii kolabo ya Zitto na Lissu ni hatari tupu

TEKNOLOJIA

JF-Expert Member
Jan 6, 2014
4,305
2,562
Kwa mara ya kwanza namwona nimemshuhudia Mwanasheria msomi kutoka Harvard Bw Andrew Chenge akibabaika baada ya kukumbana na kibano kikali cha hoja nzito kutoka kwa Zitto Kabwe na Tundu Lissu kuhusu kukiukwa kwa kanuni za bunge juu ya hoja iliyowasilishwa na wizara ya fedha na mipango.Hoja ya Zitto imepelekea kikao cha bunge kuahirishwa mpaka jioni.Hongera Zitto na Lissu,endeleeni kumfunda Bw Chenge kuhusu sheria na kanuni za bunge mpaka aelewe.CCM walidhani watawadhibiti wabunge wa upinzani kupitia tegeme lao Chenge lakini wapi,chezea Lissu na Zitto wewe,mwenyewe kanyosha mikono juu.
 
Ni nn kimetokea
Zitto alimbana MKT kuwa serikali imeleta muundo wa mpango, na sio mpango, na akanukuu vipengele vya kanuni na katiba.....Lissu akaunga mkono, Chenge akashindwa kujibu muongozo mpaka akatafakari, kambi rasmi ya upinzani upande wa bajeti ukagoma kuwasilisha ripoti yao kwa mujibu wa maelezo ya zitto na Lissu.....Chenge kafyumu akaahirisha kikao mpaka saa kumi jion
 
Tofauti yao waweke pembeni tujenge nchi yetu wote sote nawapa hongera kwa hoja nzito walizo zitoa mara nyingi huwa nasema ccm huwa hawana mda wa kufikilia vitu wanavyo wasilisha bungeni sijui huwa wanakurupuka.
 
Use your brain.zito hakusema serikali imeleta muundo wa mpango. Pia namheshim sana zito na lissu they are my favourites. Pia sio kila kitu ukijudge kwa kutumia your political wing. THERE ARE NATIONAL MATTERS NEEDING US TO UNITE
 
Ccm Taifa wanamtegemea Chenge kwa mambo mengi sana ya kisheria na hasa michoro mingi ya kifisadi.
Uwepo wa Chenge na Tulia kwenye kiti cha spika niwa kimkakati. Lakini kwa vichwa vilivyopo upinzani Ccm wanajidanganya tu. Kilichobakia kwao sasa ni kuvitaka vyombo binafsi vya Tv navyo visitishe kurusha live matangazo ya bunge.
 
Use your brain.zito hakusema serikali imeleta muundo wa mpango. Pia namheshim sana zito na lissu they are my favourites. Pia sio kila kitu ukijudge kwa kutumia your political wing. THERE ARE NATIONAL MATTERS NEEDING US TO UNITE
Sema alichosema Luteni acha maneno mengi
 
Chenge aliishia kuweweseka tuu. Kumbe hili jambo serikali walishaliona mapema na ndio maana wakaja na mkakati wa kuzuia kuonekana live. Upinzani safari hii utakuwa mwiba kwao haijapata kutokea. Naibu spika na Change badala ya kuokoa jahazi inaonyesha wanalizamisha
 
Tofauti yao waweke pembeni tujenge nchi yetu wote sote nawapa hongera kwa hoja nzito walizo zitoa mara nyingi huwa nasema ccm huwa hawana mda wa kufikilia vitu wanavyo wasilisha bungeni sijui huwa wanakurupuka.
Ccm watanzania hawajua adui yao sio wazungu, sio misaada ya nje, sio maradhi, sio ujinga Bali ni ccm! Maradhi, ujinga na umaskini ni zao LA ccm
 
E bhana hapo ndio naonaga tumepata hasara sana kumkosa pia Kafulila... ingekua 3 bomba
 
Kwa mara ya kwanza namwona nimemshuhudia Mwanasheria msomi kutoka Harvard Bw Andrew Chenge akibabaika baada ya kukumbana na kibano kikali cha hoja nzito kutoka kwa Zitto Kabwe na Tundu Lissu kuhusu kukiukwa kwa kanuni za bunge juu ya hoja iliyowasilishwa na wizara ya fedha na mipango.Hoja ya Zitto imepelekea kikao cha bunge kuahirishwa mpaka jioni.Hongera Zitto na Lissu,endeleeni kumfunda Bw Chenge kuhusu sheria na kanuni za bunge mpaka aelewe.CCM walidhani watawadhibiti wabunge wa upinzani kupitia tegeme lao Chenge lakini wapi,chezea Lissu na Zitto wewe,mwenyewe kanyosha mikono juu.
Umoja ni nguvu daima
 
Tukwambie ili iweje?nyinyi si ndio mnaoshabikia upuuzi wa serikali wa kuizuia TBC isirushe live vipindi vyote vya bunge?Subiri kipindi maalum cha bunge cha saa nne usiku labda wataonyesha.Omba Nape busara imrejee asi_edit kipande hicho cha akina Zitto.
Si ndio sasa mtwambie kichapo chenyewe,maana naona mnazunguka tu
 
Back
Top Bottom