Siielewi purport ya hii post
Yaani kuna mtu anatengeneza AI photos au vipi?
JE, NANI KAONGOPA KATI YA DKT. MWIGULU, DKT. LWAITAMA AU PROF. NDANSHAU?
Picha imevuja mitandaoni! Vijana wanasema kuwa huyo aliyevaa shati ya kijani na kofia ya njano ni Ramadhani Kailma, Mkurugenzi wa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Ila vijana wanadai kuwa huyu Kailima ni CCM lialia kama mavazi yake yanavyothibitisha na ndio maana akateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Tume ambayo itasimamia uchaguzi na kumtangaza mshindi wa Kiti cha Urais!
Ghafla kaibuka Mhe. Mwigulu Nchemba kupitia ukurasa wake wa Twita. Kakanusha na kusema kuwa huyo sio Ramadhani Kailima, bali ni Prof. Michael Ndanshau wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwa alikuwa ni mwalimu wake wa uchumi. Mwigulu anahitimisha kwa kuwataka watu waipuuze taarifa kuwa huyo ni Kailima!
Anaibuka Dkt. Azaveli Lwaitama ambaye pia alifundusha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa muda mrefu. Dkt Lwaitama anasema kuwa Prof. Ndanshau ni rafiki yake, hivyo amempigia simu kumuuliza kama kweli picha hiyo ni yake kama alivyodai Mwigulu.
Kwa mujibu wa Dkt. Lwaitama, Prof. Ndanshau ameikana picha hiyo na kuwa hakuwahi kupiga picha kama hiyo. Kwa maneno mengine, Prof. Ndanshau hakuwahi kupiga picha na Mwigulu ya aina hiyo!
Ninawafahamu wote wawili - Dkt. Lwaitama na Dkt. Mwigulu. Wote wawili tulifahamiana nao katika mazingira ya kikazi. Nakiri kuwa siwezi kusema nawajua zaidi tabia zao kwa maana sijawahi kusoma nao wala kufanya nao kazi ya kudumu zaidi ya kukutana vikaoni. Angalau Dkt Lwaitama tuliwahi kulala wote mahabusu kwa masaa zaidi ya 30 kule Butimba, Mwanza. Hii haitoshi kusema namjua fika!
Lakini nakiri kuwa simfahamu Prof. Ndanshau ingawa nimewahi kumsikia. Lakini kama ndio yule aliyekuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma au Utawala) katika Chuo Kikuu wakati huo TUDACO, huyo nimewahi kuongea naye ili kutatua tatizo la mwanachuo mmoja miaka 3 iliyopita. Kupitia mazungumzo yetu, alionekana kuwa mtu mwadilifu kwani alitoa ushirikiano wa hali ya juu sana. Mwigulu tumekutana naye kwenye vikao vya kiitifaki na hata kiibada, hivyo siwezi kusema kuwa ninamjua zaidi. Wote hao wawili kuna idara ya heshima tunazopeana!
Lakini katika hili haiwezekani wote wakasema ukweli. Ni lazima mmojawao kaongopa au kwa Kinyakyusa cha Kyela, 'alumile inongwa'! Je, ni nani anaongopa kati yao? Lakini, ni kwa nini pia aongope? Na aongope kwa maslahi ya nani? Je huyo Prof. Ndanshau yuko wapi? Je, ni kweli picha hiyo ni ya Prof. Ndanshau lakini kuamua kumdanganya rafiki yake Dkt. Lwaitama? Lakini afanye hivyo ili iweje? Je, Anaweza kujitokeza ili aukate mzizi wa fitina? Je, unajua pia kuwa mjadala huu unabeba maslahi mapana yaliyo ya kitaifa? Unafikiri kwa nini unabeba maslahi?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 14 Aprili 2025; saa 6:40 usiku