Hii kauli inapaswa kukemewa!

Hii kauli inapaswa kukemewa!

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,916
Reaction score
6,527
Nimekuwa nikisoma na kufuatilia mijadala mingi ya wananchi na wanaharakati wa masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi nk.

Wananchi na wanaharakati wengi wanaweza kukatishwa tamaa kupitia kauli za baadhi ya watu na hata viongozi.

Watu wengi wamekuwa wakitoa kauli ya "acha kulalamika, tafuta hela"
Hii kauli sio nzuri hata kidogo na inaharibu taswira nzima ya utu wa mtanzania.

Haimaanishi mtu anapodai haki au kuhoji juu ya jambo fulani, kwamba huko ni kulalamika. Inapaswa majibu sahihi yatolewe katika kujibu hoja husika!

Kauli hii inatumika maeneo mengi sana.
 
Kweli kabisa, huu upumbavu uko bongo tu hata ukisema jambo la ukweli utasikia acha makasiriko tafuta hela.
BInafsi sina tatizo kama ikitumiwa na mtu wa kawaida (rafiki, ndg) lakini inaumiza sana inapotumiwa na viongozi hasa katika maeneo ya kazi.

Ikitokea mtu anadai haki fulani inayohusu malipo, anaambiwa acha kulalamika, tafuta shughuli nyingine ya kufanya upate hela.

Kauli hii isipokemewa itatengeneza mpasuko mkubwa hapo baadae au hata kusababisha migogoro ya kiutendaji! Inapaswa kukemewa!
 
Nimekuwa nikisoma na kufuatilia mijadala mingi ya wananchi na wanaharakati wa masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi nk.

Wananchi na wanaharakati wengi wanaweza kukatishwa tamaa kupitia kauli za baadhi ya watu na hata viongozi.

Wamekuwa wakitoa kauli ya "acha kulalamika, tafuta hela"
Hii kauli sio nzuri hata kidogo na inaharibu taswira nzima ya utu wa mtanzania.

Haimaanishi mtu anapodai haki au kuhoji juu ya jambo fulani, kwamba huko ni kulalamika. Inapaswa majibu sahihi yatolewe katika kujibu hoja husika!

Kauli hii inatumika maeneo mengi sana.
Hiyo ni kauli toka Kwa Walamba asali wa CCM. Akishaondolewa mirija hawezi kutoa kauli kama hiyo. Muangalie Stroke kama anatoa tena kauli kama hiyo!
 
lanlady said:
Watu wengi wamekuwa wakitoa kauli ya "acha kulalamika, tafuta hela"

Kama mali zote unazodai kuzimiliki ulizipata ama kupitia;
  1. Wizi
  2. Uporaji
  3. UCCM
Kama nafasi zote ulizowahi kuzishika katika utumishi wa umma ulizipata ama kupitia;
  1. Rushwa
  2. Undugu
  3. UCCM
Kama mafanikio yako kimaisha yamewezeshwa kupitia ama:
  1. Unafiki
  2. Utapeli
  3. UCCM.
Kama yote hayo matatu hayakuhusu huwezi;
  1. Kuwa mwana CCM
  2. Kushabikia CCM
  3. Kutoa kauli za aina hiyo.
 
Haimaanishi mtu anapodai haki au kuhoji juu ya jambo fulani, kwamba huko ni kulalamika. Inapaswa majibu sahihi yatolewe katika kujibu hoja husika!
Mleta uzi Watanzania ki-uhalisia tumekuwa ni watu wakulalamika sana,,,,narudia tena tunalalamika sana...
Idea ya KULALAMIKA inakuja,,kwasababu tulio wengi hatupo tayari KUCHUKUA HATUA (tunataka tuonewe huruma)..
Unaambiwa UTAFUTE HELA,,kwa maana kwamba ukiwa na hela utapunguza malalamiko,,,wenye Hela hawalalamiki bali wanachukua hatua (Actions)..

Mifano General ya KUCHUKUA HATUA ni kama::

1. NATO wameiwekea vikwazo Russia,,,but Putin hajalalamika ila anachukua hatua za kupamba na vikwazo kwa mbinu mbalimbali kupunguza effect za vikwazo...
2. RUSSIA aliwafungia gas nchi za Ulaya,,, but Nchi za Ulaya hawakulalamika ila walipunguza matumizi ya gesi na kuangalia njia mbadala za kupunguza athari za kukosa gas.
3. Tanzania serikali imeweka Tozo kwa wananchi bila utaratibu wa sheria ila wananchi wamekua wanalalamika mitandaoni wakiomba waondolewe tozo.
4. Sri Lanka serikali ilishindwa kusimamia uchumi na kufanya gharama za maisha kuongezeka,, Wananchi hawakulalamika bali walichukua hatua na kuingia barabarani na kutaka Rais ajiuzulu.
5. Marekani Police walimuua yule Black,, wananchi hawakulalamika ila walichukua hatua kwa vitendo na kutaka yule police achukuliwe na hatua,,,na Serikali ikafanya hvyo
6. Tanzania Police wanaua raia, ila wananchi wanalalamika mtandaoni wakiomba iundwe tume ya kuchunguza wauaji...
 
Aina ya hizo kauli zinazotolewa kuna wakati huwa naona wanaozitoa hawajui hata wanachosema, ni kama watoto tu wanaojitafutia jibu lolote kujibu swali la msingi, hao ni wakupuuzwa, lazima tukubali upeo wetu humu ndani na kwenye jamii yetu kwa ujumla unatofautiana.
 
Mtu anakwambia hivyo halafu yeye anatembelea gari ambalo ni hela ya hao hao anaowaambie watafute hela.
 
Mchina mwenye kiwanda cha nguo pale Durban anawafanyia unyama wafanyakazi wake, wafanyakazi wale wanafanya push back na kuchoma moto kiwanda kile na kila kitu mle kiwandani, police wa kituo cha police pale Polokwane wanaua suspect, wananchi wanavamia kituo kile na kuchoma moto, mwanamke pale Tehran anakamatwa na kuuliwa akiwa in police custody, raia wanaingia mitaani na kufanya push back ya nguvu, mwekezaji wa restaurant pale Masaki ananyanyasa wafanyakazi kingono, wafanyakazi wale wanakimbilia JF kulalama, police shoot to kill suspects pale tarime, watanzania wanakimbilia in social networks kulalama, kilichobaki sasa ni kuacha kulalama na kutafuta pesa!unafiki uzuzu na uoga they got the best of us!!
 
Maisha ni vita Mura,Jikombe CCM ukomborewe Mura!
 
Attachments

  • 2938675580712793246.mp4
    4.5 MB
Mchina mwenye kiwanda cha nguo pale Durban anawafanyia unyama wafanyakazi wake, wafanyakazi wale wanafanya push back na kuchoma moto kiwanda kile na kila kitu mle kiwandani, police wa kituo cha police pale Polokwane wanaua suspect, wananchi wanavamia kituo kile na kuchoma moto, mwanamke pale Tehran anakamatwa na kuuliwa akiwa in police custody, raia wanaingia mitaani na kufanya push back ya nguvu, mwekezaji wa restaurant pale Masaki ananyanyasa wafanyakazi kingono, wafanyakazi wale wanakimbilia JF kulalama, police shoot to kill suspects pale tarime, watanzania wanakimbilia in social networks kulalama, kilichobaki sasa ni kuacha kulalama na kutafuta pesa!unafiki uzuzu na uoga they got the best of us!!
Aisee!
 
Kwamaana hiyo wasimlàlamikie W W Chebukati waingie barabarani kudai justice at any coast.
 
Back
Top Bottom