Hii 'kamata kamata' maana yake nini?

Tua Ngoma

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2015
Posts
3,365
Reaction score
8,873
Katika hali ambayo haieleweki lengo lake ni nini,kumetokea kamatakamata ya wapinzani jijini Mbeya.

Juzi usiku aliyekuwa mwenyekiti wa BAVICHA Mbeya mjini aliandika kwenye group la chama Mbeya kuhusu oparesheni UKUTA. Jana jioni amekamatwa na hajulikani yupo Kituo gani hapa Mbeya japo taarifa zinadokezwa kuwa atasafirishwa kupelekwa Dar, juzi pia aliyekuwa katibu wa Moses naye amekamatwa.

Kuna kina mama walokomenti kuhusu operasheni UKUTA taarifa zilizopo wanatafutwa na polisi na wanaishi kwa kujificha mpaka saa hii, na cha ajabu zaidi simu ya Moses haipatikani ila WhatsApp anaonekana kuwa online.

Hivi hii kamatakamata ni kwa maslahi ya nani,nani anawatuma polisi?? Rais anajua kweli kinachoendelea kwa wananchi wake au polisi wanajiamulia tu?
Polisi mnapokamata watu hovyo namna hii mnajua mnachojenga mioyoni mwa ndugu,jamaa na rafiki zao?

Jamani tusifikishane huko, nchi haiwezi endelea kwa kuwekeana visa. Kama lengo letu ni kujenga nchi lazima tukemee huu uonezi, haiwezekani watu wazibwe midomo kwa njia za kikatili. Binadamu huchoka, tuchague kufuta vyama vingi au tuache watu wafanye siasa, tuache watu waongee.

Msije sema hatukuwahi onya haya mambo
 
Tunatakiwa tusimkosoe malaika, sisi wajibu wetu ni kumsifia tu full stop
 
Word!
Ccm haikuwa tayari kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi, kinacho endelea sasa ni majibu ya hayo.
sio haikuwa tayari kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi,chama kimechoka kama mzee Kingunge alivyosema hizi ndio dalili zenyewe,hawataki kuambiwa ukweli sababu hawawezi kustahimili maumivu ya ukweli ni sawa na mfupa wa mzee ukiuvunja hauungi tena
 
Word!
Ccm haikuwa tayari kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi, kinacho endelea sasa ni majibu ya hayo.
Then wafute tu hivyo vyama,maana ndugu zetu wanapkamatwa hovyo,kuumizwa wanadhani nini wanatujengea ndugu zao,NYOYO ZA KISASI ZIKITAMALAKI NI NANI ATAPONA
 
Polisi wanatakiwa kujitafakari na kujiongeza kwani wanachokifanya sio haki kabisa ni uonevu uliopitiliza kwa upinzani.
 
Ipo siku poliCCM watasababisha nchi hii kumwaga damu.
Mi nashauri wanapokamata viongozi wakamate na ndugu zao,ili hasira zao zikaishie jela,vinginevyo sijui
 
Majizi Chadema mnajiteka ili mpate umarufu wa bure.

Juzi mmetoka kujipiga ngwala na kujiibia million 10
 
Majizi Chadema mnajiteka ili mpate umarufu wa bure.

Juzi mmetoka kujipiga ngwala na kujiibia million 10

Mnamdanganya nani??
 
Ukileta uchochezi au kuandamana unagongwa tu, kidumu chama cha mapinduzi
 
pamoja na maon hayo hata mm naunga mkono chama kmechoka na hawako tayar nch kuiweka katk demokrasia ya kweli . JE TUFANYE NN SASA MANA UKIGEUKA BOM MARA NGOMA YA MOTO KAMA MOTO BED
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…