Hii kali ''Mwanafunzi shule ya msingi ‘aloga’ walimu.......'' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii kali ''Mwanafunzi shule ya msingi ‘aloga’ walimu.......''

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Babu Lao, Jan 25, 2011.

 1. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  SHULE ya Msingi Liwiti iliyopo Tabata ipo hatarini kukosa wanafunzi baada ya wazazi kutishia kuwaondoa watoto wao kutokana na tishio la mwanafunzi mmoja kutuhumiwa kuwa mchawi.Mwanafunzi huyo wa darasa la tano anadaiwa kuwachezea wenzake kimazingara ikiwa ni pamoja na walimu na hadi sasa mwalimu mmoja wa darasa lake na wanafunzi mwenzake wanaumwa kutokana na vitisho vyake.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wanafunzi na walimu waliokataa kutajwa majina yao gazetini wamesema mwanafunzi mwenzao (jina linahifadhiwa) amekuwa akitishia maisha ya wanafunzi na walimu shuleni hapo kwa imani za kishirikina.

  Walisema hivi karibuni mwanafunzi huyo alimtishia mwalimu wake kuwa atakiona baada ya mwalimu huyo kumwadhibu mtoto huyo kwa kutofanya kazi alizopewa.

  Kwa mujibu wa wanafunzi na walimu hao, baada ya mwanafunzi huyo kuchapwa alimwambia mwalimu wake ataona kama ataamka na kwamba tangu siku hiyo (Ijumaa iliyopita) mwalimu huyo hakuonekana tena shuleni kwa maelezo kuwa anaumwa.

  Mwalimu Mkuu wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Kawo, alikataa kulizungumzia suala hilo kwa madai kuwa mpaka apate kibali kutoka kwa wakubwa zake.

  “Unajua suala hili ni la kishirikina zaidi, hivyo hatuwezi kuzungumzia masuala ya kishirikina. Tunafanya utafiti kwanza kujua ukweli wa suala lenyewe. Lakini pia siwezi kulizungumzia hadi nipate kibali kutoka kwa wakubwa wangu. Si unajua bwana mimi ni kibarua tu?” alisema mwalimu mkuu huyo.

  Mbali na mwalimu huyo kutishiwa na mwanafunzi wake na kweli akaumwa, sakata hilo halikuishia hapo kwani hivi karibuni baada ya kuchokozwa na mwanafunzi mwenzake, Warda Jamal, mwanafunzi huyo anadaiwa kumwambia ataona kama ataamka kwani atamfanyia kitu kibaya kama alivyomfanyia mwalimu wao.

  Chanzo cha habari kimesema baada ya mwanafunzi huyo kuambiwa hivyo, alienda kushitaki kwa mwalimu na ndipo mwanafunzi huyo alipoitwa na kukiri mbele ya mwalimu mkuu wa shule hiyo kuwa amekuwa akifanya ushirikina kwa msaada wa bibi yake.

  Hata hivyo, mmoja wa wazazi wa mwanafunzi aliyetishiwa aliyejitambulisha kwa jina moja la Jamal, baada ya kupata taarifa hizo, alifika shuleni hapo na kuonana na mwalimu mkuu ili kufahamu ukweli wa tukio hilo.

  Kwa mujibu wa mzazi huyo, mwalimu mkuu alimwambia hawezi kulizungumzia suala hilo hadi kwenye kikao alichokiitisha jana kati ya walimu na bibi wa kijana huyo.

  Taarifa kutoka shuleni hapo zilieleza kuwa baada ya mwalimu mkuu kumwandikia barua bibi wa kijana huyo ili afike kwenye kikao jana, alikaidi na haijafahamika uongozi wa shule umechukua hatua gani.

  Jamal, mzazi wa mwanafunzi aliyetishiwa na 'mchawi' huyo, alisema kijana wake alikuwa na hali isiyo ya kawaida kwa sababu aliumwa ghafla na kwamba inawezekana ni hofu aliyopata kutoka kwa 'mchawi' huyo.
   
 2. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Balaaa
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  this is rubbish! Hizi imani hizi kama ingekuwa ni utajiri basi tungekuwa mbali!
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,039
  Likes Received: 3,797
  Trophy Points: 280
  Hii hatari aisee!
   
 5. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,343
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Huyu bibi anafaa kuwapiga upooza mafisadi wa nchi hii ingawa nasikia wao mlingoti wao ni bagamoyo!

  Akikubali tenda sijui amwanzie nani vile???
   
 6. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,759
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Ahh huyu anafaa hawezi kuwaloga mafisadi jmn
   
 7. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,564
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hii ni joke au habari mseto??? kama ni kweli inatisha
   
Loading...