Hii itifaki imekaaje?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,227
116,839
Kuna jambo katika siasa zetu huwa likitokea huwa nabaki na maswali
na kujiuliza kila mara...

Itifaki hii imekaaje?nani ame design hii? nchi zingine nazo ni kama sisi?
au ya kwetu tu ndo iko hivi?

tumeiga wapi? China ya kikomonisti?au USSR zamani?

bado inakidhi kweli dunia ya leo?

Jambo lenyewe ni ile hali kwa mfano kuna mafuriko Dar
Rais anampa salaam za rambirambi mkuu wa mkoa wa Dar..
au kuna tukio kama la Mbwana Samata hili la juzi Rais anapeleka salaam za pengezi
kwa waziri wa burudani..

mambo yapo mengi tu huko nyuma..hadi misiba utasikia Rais anatuma
salaam za rambirambi kwa mkuu wa mkoa kuhusu vifo vya wananchi na kadhalika

Why Rais asitume salaam kwa wafiwa na wananchi moja kwa moja?
why Rais asimpe hongera mwananchi husika moja kwa moja?

Hii itifaki ikoje ikoje?

Nyani Ngabu Dark City Nguruvi3 Sibonike Pasco
 
hii ndivyo ilivyo na hata wakati wa hayati mwl nyerere ilikuwa hivyo hivyo
 
Mie nadhani itifaki ni utamaduni mnaojiwekea na kukubaliana uwe hivyo. Sidhani kama hapo kama kuna shida
 
Wewe unaona hii itifaki imekaa sawa?
wewe ukumbwe na mafuriko Rais ampe pole mkuu wa mkoa?
aliemchagua mwenyewe?
 
Tatizo stress za uchaguzi bado zinawasumbua.

Hayo yote kayafanya JK shukrani pekee mliyompa ni kumuita dhaifu... Ooh mara anashusha hadhi ya taasisi.

Kaja uso wa mbuzi kujenga heshima ya taasisi bado mambulukenge mnachonga. Mnataka nini ili mkubali kuwa taasisi inafanya kazi vzr?

Kweli magufuli mtambo maana kawafanya wakosoaji wake wakose hoja zenye mashiko kutwa nzima kujadili na kukosoa vitu vidogovidogo vya kipuuzipuuzi tu.
 
Logic ninayoiona ni kuwa tufanye mafuriko hayo yamekumba familia 200 jee Rais anaweza kutoa pole kwa familia moja moja? Pia ni kama vile RC ndio mlezi wa raia walio eneo husika hivyo pole hiyo ni kwa niaba ya wahusika kama vile Rais atoavyo pole kwa Rais wa nchi nyingine yatokeapo maafa kwao.
Ni mtazamo wangu tuu!
 
Mbona iko poa tu, we hujasikia Obama anatuma kwa rais wa ufaransa baada ya isis kufanya yao?
 
Tatizo stress za uchaguzi bado zinawasumbua.

Hayo yote kayafanya JK shukrani pekee mliyompa ni kumuita dhaifu... Ooh mara anashusha hadhi ya taasisi.

Kaja uso wa mbuzi kujenga heshima ya taasisi bado mambulukenge mnachonga. Mnataka nini ili mkubali kuwa taasisi inafanya kazi vzr?

Kweli magufuli mtambo maana kawafanya wakosoaji wake wakose hoja zenye mashiko kutwa nzima kujadili na kukosoa vitu vidogovidogo vya kipuuzipuuzi tu.
Sitafanya kosa kukuita nguruwe wa lumumba,mambo ya uchaguzi yanaingiaje humu
 
Hata leticia nyerere kafa pole anapewa mama maria nyerere mama mkwe wakati wazazi wa marehemu wapo na mumewe wa zamani madaraka yupo
 
Kuna jambo katika siasa zetu huwa likitokea huwa nabaki na maswali
na kujiuliza kila mara...

Itifaki hii imekaaje?nani ame design hii? nchi zingine nazo ni kama sisi?
au ya kwetu tu ndo iko hivi?

tumeiga wapi? China ya kikomonisti?au USSR zamani?

bado inakidhi kweli dunia ya leo?

Jambo lenyewe ni ile hali kwa mfano kuna mafuriko Dar
Rais anampa salaam za rambirambi mkuu wa mkoa wa Dar..
au kuna tukio kama la Mbwana Samata hili la juzi Rais anapeleka salaam za pengezi
kwa waziri wa burudani..

mambo yapo mengi tu huko nyuma..hadi misiba utasikia Rais anatuma
salaam za rambirambi kwa mkuu wa mkoa kuhusu vifo vya wananchi na kadhalika

Why Rais asitume salaam kwa wafiwa na wananchi moja kwa moja?
why Rais asimpe hongera mwananchi husika moja kwa moja?

Hii itifaki ikoje ikoje?

Nyani Ngabu Dark City Nguruvi3 Sibonike Pasco
Nadhani sio kila itifaki lazima tuige mahali, kila jambo lina mkuu husika na wizara husika, hivyo rrais yuko responsible kwa mkuu husika au wizaa husika, kama ni michezo, kwa waziri wa michezo kisha mchezaji husika, kama ni majanga, kwa mkuu wa mkoa husika kisha wahanga.

Pasco
 
Kukariri nako ni janga la taifa! Itifaki unayotaka kama imeandikwa mahali, ebu tuambie ni wapi imeandikwa hivyo! Kama yeye mhusika ameamua kutumia itifaki hiyo, basi kwake iko sahihi'
 
Tatizo mna stress hadi mnatia huruma
Stress za nini?tunakula,tunakunywa,tunalala,watoto wanaenda shule,hatujagombea hata udiwani na sio wanasiasa,hapa tunataka kuongeza ufahamu tu.tatizo kuna majitu kama nyie bado mko kwenye kampeni mtakufa masikini kwa ujinga
 
We huonagi mashabiki wa soka wanavyougulia maumivu wakati kocha na wachezaji wakiwa wanafurahia maisha?

Tatizo siasa mmezigeuza kama ushabiki wa mpira.... Kisa hujampigia aliyeshinda basi kutwa nzima ni kukosoa hata vitu vya kipuuzi mradi uhalalishe na kuwaaminisha watu kuwa maamzi yako kabla ya kupiga kura ndo yalikua sahihi...

Ni kama vile bado mnaishi kwenye ndoto za uchaguzi.

Poleni sana.
 
Back
Top Bottom