Hii itawauma wengi

Hii itawauma wengi

Nelson Kileo

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2011
Posts
3,054
Reaction score
3,263
Sielewi kama mimi ndio nina matatizo ama vipi, maana hivi vitu watu wanafanya siku hizi vinanichanganya

Unakuta mtu ana miaka 25+ anaishi nyumbani kwao, hata rent ya miezi miwili hawezi kujilipia lkn ukija kwenye status yake unakuta yy ni bingwa wa kuandika historia ya mabilioni ya Jeff Bezos, Jack Ma na kina Patrice Motsepe

Mtu huyo huyo hafanyi chochote kbs, akishashiba chakula cha mama anakuja IG anaandika "Dear haters, the more you hate me the more I become successful" Ni kama vile kuwa na haters ni fashion inayoTrend

Watu wa aina hii ukimuuliza bruh mishe zinaendaje,kwanza lazima akujibu kwa kingereza,utasikia "Patience bruh, you know patience is bitter, but it's fruit is sweet". Sasa mimi najiuliza hivi tatizo ni kuwa na elimu au kutokuwa na elimu. Maana watu wa namna hii huwa wanasoma vitabu kweli kweli, cashflow quadrant yote ipo kichwani

Kukaa nyumbani kufikiria kuwa milionea ni utoto sana na hii michezo ya kujifanya wasomi na wachambuzi haitatufikisha popote pale. Mtu anajua matoleo yote ya Range Rover lkn bado nauli ya daladala mpk aombe kwa mtu

Sisemi kuwa watu wasiwe na ndoto kubwa, hapana! lkn kabla ya kutamani kuwa bilionea fikiria kwanza jinsi utakavyofanikisha kuhamia kwako. Kama una degree ya BaEd na hauna ajira, nunua mabenchi fundisha watoto twisheni jioni, 25,000 kwa mwezi, anza na watoto 10, hiyo ni 250,000... hapo unaweza kuanzisha baby care ya wanafunzi 40, kila mmoja ada 30,000 kwa mwezi una milioni yako. Asubuhi baby care, jioni twisheni, weekend mitihani

Muhimu sana ukaepuka kuwaambia watu shida zako, coz kila mtu ana shida zake kibao na hkn anayeshtushwa na shida zako. Km una ndoto sahau mtu kuinvest hela yake kwenye ndoto yako wkt ww haujainvest hata mia. Komaa invest hela yako then push, mtu akitaka kukujoin akukute kati kati, ht ukimwambia inahitajika mil 20 at least inaelezeka hiyo hela itatumika wapi. Sio uniombe mil 5 wkt unalala kwa mama'ko, hapo nitajua tu huyu jamaa hela yng atalipia kodi....#NIMEIKUTA MAHALI WADAU#
 
Mkuu kiuhalisia maisha hayapo hivyo aisee,wewe pambana tu na hali yako,hautakiwi kuishi kwa ajili ya watu wengine,ishi kwa ajili yako na utafanikiwa,kukaa na kuumiza kichwa juu ya nani anaishi wapi na anafanya nini wakati wote mnapambania ku`survive,huo nao ni ujinga kama ujinga mwingine,utacheleweshwa sana ukianza kuumiza kichwa kwa ajili ya watu wengine wanavyoishi,pole sana!
 
Kuna kitu kinaitwa udhubutu. Vijana wengi wa kibongo hatuna hii kitu..
Yaan kudhubutu kutoka kwenu na kufanya kaz fulani...
Kudhubutu kutoka kwenu na kwenda kufanya kufanya shughul japo uingize chochote..

Kinacho waponza watu ni ile hali ya kuwa nitaonekanaje na usomi wangu huu nikianza kufanya kaz fulani.
 
Tena watu kama hao unakuta anapata tubinti tuzuri tu na unakuta ana watoto hata watatu au wanne kila mmoja ana mama yake, unabaki unashangaa wewe mchapa kazi mpaka miaka 30 bado huna mtoto hata mmoja na hujapata hata rafiki wa maana
 
Sielewi kama mimi ndio nina matatizo ama vipi, maana hivi vitu watu wanafanya siku hizi vinanichanganya

Unakuta mtu ana miaka 25+ anaishi nyumbani kwao, hata rent ya miezi miwili hawezi kujilipia lkn ukija kwenye status yake unakuta yy ni bingwa wa kuandika historia ya mabilioni ya Jeff Bezos, Jack Ma na kina Patrice Motsepe

Mtu huyo huyo hafanyi chochote kbs, akishashiba chakula cha mama anakuja IG anaandika "Dear haters, the more you hate me the more I become successful" Ni kama vile kuwa na haters ni fashion inayoTrend

Watu wa aina hii ukimuuliza bruh mishe zinaendaje,kwanza lazima akujibu kwa kingereza,utasikia "Patience bruh, you know patience is bitter, but it's fruit is sweet". Sasa mimi najiuliza hivi tatizo ni kuwa na elimu au kutokuwa na elimu. Maana watu wa namna hii huwa wanasoma vitabu kweli kweli, cashflow quadrant yote ipo kichwani

Kukaa nyumbani kufikiria kuwa milionea ni utoto sana na hii michezo ya kujifanya wasomi na wachambuzi haitatufikisha popote pale. Mtu anajua matoleo yote ya Range Rover lkn bado nauli ya daladala mpk aombe kwa mtu

Sisemi kuwa watu wasiwe na ndoto kubwa, hapana! lkn kabla ya kutamani kuwa bilionea fikiria kwanza jinsi utakavyofanikisha kuhamia kwako. Kama una degree ya BaEd na hauna ajira, nunua mabenchi fundisha watoto twisheni jioni, 25,000 kwa mwezi, anza na watoto 10, hiyo ni 250,000... hapo unaweza kuanzisha baby care ya wanafunzi 40, kila mmoja ada 30,000 kwa mwezi una milioni yako. Asubuhi baby care, jioni twisheni, weekend mitihani

Muhimu sana ukaepuka kuwaambia watu shida zako, coz kila mtu ana shida zake kibao na hkn anayeshtushwa na shida zako. Km una ndoto sahau mtu kuinvest hela yake kwenye ndoto yako wkt ww haujainvest hata mia. Komaa invest hela yako then push, mtu akitaka kukujoin akukute kati kati, ht ukimwambia inahitajika mil 20 at least inaelezeka hiyo hela itatumika wapi. Sio uniombe mil 5 wkt unalala kwa mama'ko, hapo nitajua tu huyu jamaa hela yng atalipia kodi....#NIMEIKUTA MAHALI WADAU#
Iko deep sana mkuu........ambaye hajakuelewa kichwa ngumu.
 
Hata humu JF wapo wengi mno. Hujifanya wajuzi, wachambuzi na wenye kashfa nyingi mno.
Hii yote ni athari ya utandawazi wa teknolojia na haja ya walimwengu kuishi zaidi kwa kuridhisha waliowazunguka kuliko uhalisia wa maisha yao.
Ni mbaya kwa mtu kuwa muongo lakini ni mbaya zaidi kuamini uongo wako mwenyewe kuwa kweli. Mtu anajiaminisha kuwa ni 'star' wa kwenye mtandao kwa picha alizopiga kwenye gari ya mjomba huku akiishi sebuleni kwa shangazi kupelekea kutotaka chochote chini ya kile anachojinasibu juu yake kwa hofu ya 'mahaters' wa mtandaoni. Athari yake anachagua kazi ilhali hana uwezo wa maisha anayojifanya kumiliki.
 
Unawaskiliza motivation speaker hahahaha wenzetu wazungu wanamuandaa mtoto tangu mdogo wanamtunzia pesa akifikia umri flani wanamtaftia kazi au biashara huku ile pesa anapewa ajitaftie kiukweli sidhani kama wanapenda kukaa home ila wakaibe msiwape pressure sana hwa vijana tunatengeneza taifa la watu wenye roho mbaya
 
Back
Top Bottom