Hii isomwe na wanaume tu

Hii isomwe na wanaume tu

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,614
HII ISOMWE NA WANAUME TU

Wanaume wenzangu, tufanye kazi kwa bidii tutafute hela ili uzee wetu tuwe na uwezo wa kujitegemea. Hakikisha kwenye uzee wako una pesa zako mwenyewe za kukufanya usurvive. Sahau kuhusu watoto, na mama yao kwamba watakutunza. Wewe ndiye stranger pekee kwenye hiyo familia unayoiita ya kwako. Hiyo nyumba ni ya huyo mwanamke na watoto wake. Not yours.!

Babu yangu aliniambia kwamba mwanaume aliyeoa ni sawa Tingatinga, ambalo linatengeneza Barabara, lakini ikishakamilika linabebwa juu juu kwenye Lori na kuondolewa, eti likitembea litaharibu barabara. Yani barabara ambayo Tingatinga lenyewe limeitengeneza haliruhusiwi kutembea juu yake.

Vivyo hivyo kwa mwanaume aliyeoa. Atajinyima, atajishughulisha, atajizuia kufanya anasa, atakopa, atavaa mitumba ili tu watoto wake waishi vizuri, wale vizuri na kusoma shule nzuri. Siku hizi urithi pekee uliobaki ni elimu bora coz mashamba ziliishaga. Lakini pamoja na yote hayo, bado ukizeeka hao watoto sio wako, ni wa mama yao. Wewe watakuita "Kamzee".

Watoto wakiwa na umri wa miaka 10 ndipo mama yao anaanza kuwajaza taarifa zisizovutia kuhusu wewe. Kadri wanavyokuwa ndivyo wanavyoelezwa mambo mengi. Wakifika utu uzima atawaambia "isingekua mimi hamgesoma, yeye alikua ni pombe tu na wanawake" Ukisikia hivyo ujue tingatinga limemaliza kazi yake sasa linakaribia kuondolewa barabarani.

Watoto wanapoanza kazi, mzee anakua amestaafu. Wanapokuja kutembelea wazazi, wakiondoka wanampa baba elfu 5 mbele ya mama. Halafu wanaenda jikoni na mama, wanampa hela kwa siri bila mzee kujua. Wakiondoka mama anamfuata mzee na kumwambia sukari imeisha. So ni suala la mzee kuamua kutoa ile elfu 5 aliyoachiwa na watoto ikanunue sukari, otherwise anywe chai isiyo na sukari. Hii ni moja ya sababu inayowafanya wazee kufa mapema baada ya kustaafu na kuacha wake zao Wajane.

Nimeshuhudia wazazi wenye watoto ng'ambo wakimchukua mama yao akaenjoy life majuu, na kumuacha baba yao nyumbani akilisha Ng'ombe wao wawili, na kutafuta chakula cha kuku.!

Wanaume work hard and save something for yourself at old age. Tafuta pesa kwa bidii, wape watoto elimu bora, wape mahitaji yao muhimu, jenga nyumba nzuri waishi vizuri, lakini ukizeeka dont expect too much from them. Enjoy maisha ya uzee kwa pesa zako mwenyewe ulizochuma ujanani.

"Hii ni siri wewe ukiwa kama mwanaume usiache kushare ujumbee huu na wanaume wenzako waone.
 
Tatizo nyie wanaume enzi za ujana wenu mnahangaisha wanawake na michepuko mpaka wanakoma na wanabaki kuhangaika na watoto most of the time wenyewe, mkishakuwa wazee hamwezi kufanya kitu mnaangalia huruma za watoto, mnadhani watoto hawaoni mnayoyafanya? Mfano Baba Diamond, wengi wenu mko kama yeye, mko majumbani kama picha tu.
A happy home is when mommy is happy first,
 
1149865
1562677300358.png
 
*HII ISOMWE NA WANAUME TUU*


*Wanaume wenzangu, tufanye kazi kwa bidii tutafute hela ili uzee wetu tuwe na uwezo wa kujitegemea. Hakikisha kwenye uzee wako una pesa zako mwenyewe za kukufanya usurvive. Sahau kuhusu watoto, na mama yao kwamba watakutunza. Wewe ndiye stranger pekee kwenye hiyo familia unayoiita ya kwako. Hiyo nyumba ni ya huyo mwanamke na watoto wake. Not yours.!*

*Babu yangu aliniambia kwamba mwanaume aliyeoa ni sawa Tingatinga, ambalo linatengeneza Barabara, lakini ikishakamilika linabebwa juu juu kwenye Lori na kuondolewa, eti likitembea litaharibu barabara. Yani barabara ambayo Tingatinga lenyewe limeitengeneza haliruhusiwi kutembea juu yake.*

*Vivyo hivyo kwa mwanaume aliyeoa. Atajinyima, atajishughulisha, atajizuia kufanya anasa, atakopa, atavaa mitumba ili tu watoto wake waishi vizuri, wale vizuri na kusoma shule nzuri. Siku hizi urithi pekee uliobaki ni elimu bora coz mashamba ziliishaga. Lakini pamoja na yote hayo, bado ukizeeka hao watoto sio wako, ni wa mama yao. Wewe watakuita "Kamzee".*

*Watoto wakiwa na umri wa miaka 10 ndipo mama yao anaanza kuwajaza taarifa zisizovutia kuhusu wewe. Kadri wanavyokuwa ndivyo wanavyoelezwa mambo mengi. Wakifika utu uzima atawaambia "isingekua mimi hamgesoma, yeye alikua ni pombe tu na wanawake" Ukisikia hivyo ujue tingatinga limemaliza kazi yake sasa linakaribia kuondolewa barabarani.*

*Watoto wanapoanza kazi, mzee anakua amestaafu. Wanapokuja kutembelea wazazi, wakiondoka wanampa baba elfu 5 mbele ya mama. Halafu wanaenda jikoni na mama, wanampa hela kwa siri bila mzee kujua. Wakiondoka mama anamfuata mzee na kumwambia sukari imeisha. So ni suala la mzee kuamua kutoa ile elfu 5 aliyoachiwa na watoto ikanunue sukari, otherwise anywe chai isiyo na sukari. Hii ni moja ya sababu inayowafanya wazee kufa mapema baada ya kustaafu na kuacha wake zao Wajane.*

*Nimeshuhudia wazazi wenye watoto ng'ambo wakimchukua mama yao akaenjoy life majuu, na kumuacha baba yao nyumbani akilisha Ng'ombe wao wawili, na kutafuta chakula cha kuku.!*

*Wanaume work hard and save something for yourself at old age. Tafuta pesa kwa bidii, wape watoto elimu bora, wape mahitaji yao muhimu, jenga nyumba nzuri waishi vizuri, lakini ukizeeka dont expect too much from them. Enjoy maisha ya uzee kwa pesa zako mwenyewe ulizochuma ujanani.*
*"Hii ni siri wewe ukiwa kama mwanaume usiache kushare ujumbee huu na wanaume wenzako waone.
😂😂😂😂😂
Umenichekesha saana ila umeongea ukweli saana wamama ndio tabia zao kusema habari mbaya za wababa kwa watoto..
Yani kuwajaza sumu watoto wamjali yeye sio baba yao🤝🤝🤝
 
Kwahiyo mnataka kusema kwamba wake zenu wanayowaambia watoto wenu ni ya uongo? Yaani wanaume bwana

Badala ya kuacha hayo maovu mnayoyafanya mnabaki kutupa lawama kwa wanawake wanawaowaambia watoto ukweli kuhusu maovu yenu eti kwa sababu tu mnajinyima kuwahudumia

Sasa kwani mkifanya hivyo mnakuwa mmewafanyia favour si ni jukumu lenu kufanya hivyo au? Wanaume kujinyima na kuhudumia familia siyo ticket ya ninyi kufanya maovu mnavyojisikia

Na mtaendelea kulalamika na kulaumu hivyo hivyo hadi mwisho wa dunia si hamtaki kubadilika eti mnadhani sijui kupiga na kusepa au kuzalisha na kuacha ndo suluhisho basi endeleeni kufanya hayo halafu tuone mwisho wake maana badala ya kutafuta suluhisho mnatafuta mshindi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom