Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,723
Wakuu habari, nimeshindwa kumuelewa huyu jamaa hii alama sign yake kutokana na tafsiri yangu niliyoipata miaka kadhaa.
Miaka minne iliyopita nilikuwa na mwanaJF tukitoka Sinza kuelekea Ukonga, tulipofika Buguruni Sokoni jamaa akasema tukale maana anasikia njaa. Akanipeleka Bar moja hapo hapo sokoni ina jina kama la wodi moja ya Muhimbili. Sikuvutiwa na mazingira ya pale hivyo sikula wala kunywa chochote.
Nilishangaa kuona mijimama ikiwa ndani ya Dera ikipita pita, kumbe ilikuwa inauza tupu mchana ule wa saa tisa.
Kuna mmoja alinikata jicho,kutokana na aibu nilonayo nikawa natizama chini.Kuna wakati nami nikamkata jicho akanionesha hiyo ISHARA kama ya Bob Junior mie nikatikisa kichwa kuashiria sitaki.
Nikamuuliza mwenyeji wangu ishara ile anamaanisha nini maana nilivyoona vidole vitatu vimesimama na viwili vimejikunja na kushikana nikajua anamaanisha 3,000, kumbe sivyo alikuwa anamaanisha anatoa jicho (Maumbile na Kinyume). Niliogopa sana na kusisitiza tuondoke eneo lile fasta.
Swali langu:
Ina maana Bob Junior anatoa jicho au ni matumizi ya ishara pasipokujua matumizi yake?
Je, hiyo ishara ina maana zaidi ya moja tofauti na niijuayo mimi kwa mazingira ya TZ?