Hii interview ya Rightway Primary school inatesa watoto

Hii interview ya Rightway Primary school inatesa watoto

Kwani lazima aende right way?
Kwanza kabisa mtoto chini ya miaka kumi hawezi ku concentrate for two hours non-stop. Hiyo shule Ni ya CCM?
Walimu wa hapo hawajasoma saikolojia ya watoto kabisa.
It is a wrong school. Achana nayo
Tunahukumu vibaya kwa kukosa taarifa sahihi toka upande wa shule.

Kuna mdau kafafanua hiyo shule wanapima watoto na tabia zao, hivyo katika hayo masaa mengi wanakuwa wanacheza tu huku wanamsoma character zake, kama mbaya wanamkataa hata kama mitihani ya taaluma kapa 100% yote.
 
Hiyo ni private school, hapo mbali na mtihani lakini wana muda wa kuwafanyia watoto observation especially kwenye social behaviours, kuna short break ya tea,

Kuna shule ambazo mtoto anaingia anafanya pepa faster unaondoka nae, lakini kwa rightway utaratibu wap ni tofauti na ni mzuri, nina mtoto wa causin wangu anasoma hapo

Akifaulu interview Monday utamlipia 20,00p anashinda shule kwa ajili ya total observation kama tabia zake zitakua mbovu watakwambia kwamba ondoka na mwanao, lakini kama atakua na tabia njema watakwambia ukalipe ada
Wanaletewa watoto ili wawafundishe sasa wao wanataka watoto walio kwishafundishwa?
 
Mtoto mdogo anafanya Interview ya nini ila wazazi nao ni mabwege sana
 
Kumbuka kigezo cha shule nzuri ni matokeo, lazima wafanye hivyo ili wapate cream, vilaza wawapige chini.
Unajuaje kama mtoto mdogo ni kilaza au sio kilaza.. Mtu ubongo unakamilika kujua akifikisha miaka 10..
 
Wanaletewa watoto ili wawafundishe sasa wao wanataka watoto walio kwishafundishwa?
Hawawezi kupokea mtoto ambae anakuja kuvuruga wenzie wote.
Malezi huanzia nyumbani kwanza kama ana msingi wao wanaenda kuendeleza na kuvinoa(refine and sharpen) vipaji vyake.
 
Aisee kumbe hadi Nursery wana interview
 
Tunahukumu vibaya kwa kukosa taarifa sahihi toka upande wa shule.

Kuna mdau kafafanua hiyo shule wanapima watoto na tabia zao, hivyo katika hayo masaa mengi wanakuwa wanacheza tu huku wanamsoma character zake, kama mbaya wanamkataa hata kama mitihani ya taaluma kapa 100% yote.
Nilishaanza kuhukumu. Duh afadhali umefafanua
 
Nilishaanza kuhukumu. Duh afadhali umefafanua
Siyo kosa lako bali namna alivyoleta taarifa hii huyu mleta thread.

Inaonekana jamaa hakuelewa sababu na nini kinaendelea muda wote huo au anajua ila kaumizwa na mwanawe kukataliwa hiyo shule, kwa hivyo kuweka hapa hivi ni kisasi dhidi ya shule.
 
Leo ni siku ya interview hapa Rightway Nursery and Primary school, Mbezi .
Haiwezekani mtoto wa lower primary school(std 1-3) afanye mtihani kuanzia saa 2 Asbh mpk saa 7 mchana . Mtoto anatahiniwa masomo 4 .Wakati zamani kwenda form one unatahiniwa masomo 2 tu, Hesabu na Kiingereza.
Naomba wizara ya Elimu ifatilie hili Jambo. Yaonekana hIzi english medium schools haziratibiwi ipasavyo.
Ifungieni kama Mlivyofanya kwa ST JUDE, nyie MATAGA
 
Siyo kosa lako bali namna alivyoleta taarifa hii huyu mleta thread.

Inaonekana jamaa hakuelewa sababu na nini kinaendelea muda wote huo au waanajua ila kaumizwa na mwanawe kukataliwa hiyo shule, kwa hivyo kuweka hapa hivi ni kisasi dhidi ya shule.
Mtoto wake atakua Ni wale wanaoitwa "junior" hamna nidhamu, malezi Ni ziro sasa akiachwa acheze na wenzake kwasababu Hana good manners anagombana nao. Keep it up Rightway.
Kina junior Tena wenyewe wanaita junio wakae kando.
 
Hawawezi kupokea mtoto ambae anakuja kuvuruga wenzie wote.
Malezi huanzia nyumbani kwanza kama ana mwingi wao wanaenda kuendeleza na kuvinoa(refine and sharpen) vipaji vyake.
Wawapunguzie ada watoto wanaofaulu sababu wazazi wao tayari wameshafanya kazi kubwa. Siyo kuwaadhibau wazazi kwa ada kubwa.
Hao wanachukua Top layers ili ziwasaidie ku brand biashara yao
 
Wawapunguzie ada watoto wanaofaulu sababu wazazi wao tayari wameshafanya kazi kubwa. Siyo kuwaadhiba wazazi
wapunguze vipi wakati walimu wanalipwa vizuro, shule ipo vizuri sana na wameweka ada kubwa ili wapate wenye nia ya kusomesha hapo?
 
wapunguze vipi wakati walimu wanalipwa vizuro, shule ipo vizuri sana na wameweka ada kubwa ili wapate wenye nia ya kusomesha

Wawapunguzie ada watoto wanaofaulu sababu wazazi wao tayari wameshafanya kazi kubwa. Siyo kuwaadhibau wazazi kwa ada kubwa.
Hao wanachukua Top layers ili ziwasaidie ku brand biashara yao
Hizi shule za kisasa ukiweka ada ndogo hupati watoto.
Wewe unataka mama zao waweke wapi sura zao wakifika kitchen party au salon.
Wengine wanatamba kabisa " mie mwanangu anasoma englishit au Franshit international nursery academy ada milioni tatu laki Tisa."
Mwingine atatamba mwanangu anasoma St. Toiletick international educational institute ada milioni mbili kwa semester.
Nursery nako siku hizi Kuna semester.....
 
na kuna watu hizo milioni 3 kwa siku wanaingiza kwenye biashara zao, wengine ni wabunge kwa mwezi anaingiza zaidi ya milioni 13 sasa akitoa milioni 3 anabaki na milioni 10 kwa mwezi, ndio maana KILA MBUZI ALE USAWA WAKAMBA YAKE.
 
Leo ni siku ya interview hapa Rightway Nursery and Primary school, Mbezi .
Haiwezekani mtoto wa lower primary school(std 1-3) afanye mtihani kuanzia saa 2 Asbh mpk saa 7 mchana . Mtoto anatahiniwa masomo 4 .Wakati zamani kwenda form one unatahiniwa masomo 2 tu, Hesabu na Kiingereza.
Naomba wizara ya Elimu ifatilie hili Jambo. Yaonekana hIzi english medium schools haziratibiwi ipasavyo.
😃😃😃 Yaan katoto ka 1-3 kana pigwa interview jaman haya ni maajabu binafsi nayaona embu naomba nijuze interview ya watoto wa umri huo una husisha nini hasa ?
 
Kumbuka kigezo cha shule nzuri ni matokeo, lazima wafanye hivyo ili wapate cream, vilaza wawapige chini.
Shule nzuri inapika wanafunzi yenyewe sio kudandia tu watoto vichwa alafu wajewajichukulie sifa na utukufu wao
 
Back
Top Bottom