Hii inshu ni yakweli au natapeliwa???

Hii inshu ni yakweli au natapeliwa???

Superboy

Member
Joined
Sep 17, 2013
Posts
45
Reaction score
6
Kuna mdada msenegal kaniomba msaada. Yeye ni yatima baba yake enzi za uhai alikuwa mfanya biashara wa madini katika maswala ya urithi aliandikwa yeye. Sasa kuna pesa ziko scotland 4200000 milion dolla na sheria za benki zinamtaka atafute mtu ambaye sio wa senegal ndio atumiwe hizo hela na mdada kanipoint mimi halfu wanataka hati ya kiapo kutoka kwa mwanasheria wa senegal nilipata anwani ya mwanasheria wa senegal kutoka kwa huyo mdada mwanasheria anataka $700 ili aandike hiyo hati ampe huyo mdada asaini halafu aitume bank ndio wanitumie hizo hela ili yule mdada aje tanzania aendelee na masomo nayule mdada hana hiyo $700 na nilipo wasiliana na bank wakasema wakiipata tu hiyo hati baada ya lisaa wananitumia hiyo hela 4.2us dollas na yule mwanasheria anadai nimtumie western union ili aikamilishe hiyo hati sasa nitume au. Halafu wanaotaka niwasaidie inshu kama hii wanazidi kila kukicha.
 
kaka achana kabisa na hilo janga! utakuja hapa hapa jf kutulilia umetapeliwa...pole sana na achana kabisa na hiyo ishu/inshu!
 
Wewe mgeni?,achana nao hao matapeli wa 419 scam,ukiendelea kuwachekea wanakulipua sasa hivi!,ikiwezekana watukane kabisa hawatakutumia tena
 
Ukizubaa kidogo tu unakatwa,hao matapeli ndugu yangu kimbia kabla haujaliwa
 
Nimegundua wewe ni mgeni kwenye mambo ya kutumia mitandao, mimi nilishahawahi kupata msg kama hizo kama mara mia hivi, huwa nawatukana kistaarabu. Nakuomba achana nao kabisa na usithubutu hata kuwatumia account namba zako, kama unaona tunakuonea wivu fanya wanavyotaka ila usirudi humu jf kuwaomba ushauri kwani tutakutana mitusi ya nguoni halafu uanze kulalamika kuwa jf imekuwa kama facebook
 
We umekuja dunian hiv karibuni ee?
Hiyo michezo yakitambo sana usijaribu.Au wasiliana na Msamiati akushilikishe alichokifanya
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hivi umeishajiuliza huyo binti amekujuaje? Kama haujajiuliza hilo swali na kupata jibu peleka hiyo dola 700 halafu urudi hapa JF kutupa story.

Achana nao.

Tiba
 
Utasubiri hela hadi jua lizame...fanya kazi ndg yangu achana na mawazo na huo mkondo wa matapeli.
 
unahamu ya kukatwa mkuuu,.... achana na hawa matapeli wewe....
 
Kuna mdada msenegal kaniomba msaada. Yeye ni yatima baba yake enzi za uhai alikuwa mfanya biashara wa madini katika maswala ya urithi aliandikwa yeye. Sasa kuna pesa ziko scotland 4200000 milion dolla na sheria za benki zinamtaka atafute mtu ambaye sio wa senegal ndio atumiwe hizo hela na mdada kanipoint mimi halfu wanataka hati ya kiapo kutoka kwa mwanasheria wa senegal nilipata anwani ya mwanasheria wa senegal kutoka kwa huyo mdada mwanasheria anataka $700 ili aandike hiyo hati ampe huyo mdada asaini halafu aitume bank ndio wanitumie hizo hela ili yule mdada aje tanzania aendelee na masomo nayule mdada hana hiyo $700 na nilipo wasiliana na bank wakasema wakiipata tu hiyo hati baada ya lisaa wananitumia hiyo hela 4.2us dollas na yule mwanasheria anadai nimtumie western union ili aikamilishe hiyo hati sasa nitume au. Halafu wanaotaka niwasaidie inshu kama hii wanazidi kila kukicha.

Imeandikwa utakula kwa jasho. Mdogo wangu kimbia, utakuja mwaga kilio. Watu wako kazini hapo !!!
Nshatumiwa nyingi kama hizo miaka kama mi 5 iliyopita. Wazee waku chanja hao, it seems kijana bado maisha hujayaona kabsa.
Ila tusikukatishe tamaa kama vipi we watumie mpunga huo ujitwalie mamilioni hayo kisha uje kuntoa msimbazi wa soda !!!
 
Mimi nimeshaliwa sema ilikuwa dola mia tu mambo ya kwenye mitandao wewe jaribu nawewe uone yani hakuna cha bank wala nini ni software tu wanatengeneza report za bank wewe utalizwa dola 700 ni nyingi
 
Mkuu! Shaulilo!! Umedandia gari kwa mbele nakwambia yani umefanya hadi hayo maprocess? Duu!! Mwenzako nilipewa gia hizohizo nikashtuka na kushtuliwa mapemaaaa! Sasa we toa hiyo akaunti yako ! Zingatia ushauri wa wadau! Ukiona wanakuonea wivu endelea ila uturejeshee feeback hapa!!
 
Andika jina la baba yake huyo binti ktk mtandao uone mambo!? UTAPELI HUO '419 SCAM' andika hv ktk mtandao uone mambo! Hiyo Avatar ya huyo demu ni 'FAKE' Ni Wanaigeria wanaofanya UPUMBAVU HUO! ACHA KABISA! KAA KMYA
 
Bila shaka baba anaitwa Dr Phillip Desmund! Usinambie nimejuaje! Achana nao
 
Back
Top Bottom