Hii inaweza kuwa sababu mbaya/ovu kabisa ya kuua binadamu mwenzio

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Al Sudy alikuwa ametulia kwenye kiti chake akiwa anabembea. Ni aina ile ya viti hufahamika kama swing chair.au kiti bembea. Pembeni yake alikuwa kisahani cha kuzimia sigara na sigara ikiwa inateketea taratibu katikati ya vidole vyake viwili.

Akienda mbele na kurudi nyuma huku usoni akiwa amechora tabasamu pana na wakati mwingine kicheko kikitoka taratibu. Usoni na moyoni pia anaonesha kuwa na furaha macho yake yakikodolea mwanamke mrembo aliyekuwa mbele yake.

Al Sudy alikuwa mkimya sana eneo lile.hakuwa na marafiki wengi sana.tofauti na wenzake wengi eneo lile walipenda mara nyingi jioni kujumuika kunywa kahawa.yeye alikuwa akirudi kwake anatulia ndani na kunatawaliwa na ukimya mkubwa.

Siku hiyo jirani alisikia kelele kidogo za mwanamke akilia halafu kukawa na ukimya.lakini kuna vitu vilisikika vikianguka kama sahani au vikombe vya udongo.

Jirani alipiga simu haraka polisi kutoa taarifa kuwa kuna shida nyumba ya jirani. Dubai haina sana foleni. Baada ya kugonga sana polisi wanaingia. Ndo wanamkuta Al Sudy akiwa katika hali hiyo.

Mbele yake yupo mwanadada mrembo ametulia tuli. Hana shida katulia sana huku akiwa hana hata nguo moja. Polisi wanapoangalia zaidi wanaona kichwa cha msichana yule mrembo kimekaa pembeni ya ubavu wake wa kushoto.

Huwezi ukadhani hii ni aina mpya ya sarakasi.maana damu nyingi inaonekana pembeni. Polisi wakiwa wamelekeza bastola zao uelekeo aliopo Al Sudy. Pembeni wanaona kuna Jambia limeloana damu. Al Sudy wala hashtuki.

Miezi kadhaa baadaye inakuja kufahamika mle ndani kuna vichwa vya binadamu 14. Miili yao haionekani.vichwa hivi vimehifadhiwa kwenye jokofu.

KWA NINI AL SUDY ALIUA WATU HAWA WOTE KWA KUWAKATA VICHWA?

JIBU
lake lilikuwa jepesi sana. "I killed them to watch them dying"
"Nliwaua kuwatizama wakifa"

Alitumia lugha yake ya kiarabu.baada ya mahojiano alikuja funguka kuwa binafsi anaenjoy sana kutizama mtu anayekata roho kwa maumivu.huwa anajisikia raha asiyoweza kuileza.hivyo huua kuangalia jinsi watu wanavyokufa.though katika kusindikiza hilo huwatafutia sababu nyingine moja wapo ni kuwa watu hao wamemwasi mungu. Mfano huyu wa mwisho alikuwa mwanamke wa kiarabu ambaye alikubaki kuzini naye.kitu ambacho ni kosa kiimani.hilo lilimpa faraja kuwa hana dhambi.

Hivyo ili kupata uhakika wa dhambi hiyo alimwambia kama anataka apigwe mti avue nguo. Ni Latifa alivua na kuwa tayari kwa tendo hilo ndipo alipomsukuma chini na kuangusha vyombo. Akamwahi akamziba mdomo na kumkata koromeo lake changa....

Anasema alikuwa anajisikia raha kuona roho ikitengana na mwili.hapo alipuliza moshi wa sigara ukaenda hewani ukapotea na roho ya bi latifa.

Nikawaza. Kuna sababu gani ovu na katili ya kumuua mtu zaidi ya kumuua ili umwangalie anavyokufa?
 
.....Mapepo yanamsumbua , MTU safi uwezi ona damu ya binadamu ukakenua mineno ya njano
NB: Uchungu wa kumegewa mke unaweza kuua kinyama kuliko huyo Al sudy mrembo.
 
Hili halihusiani na imani..ni akili zake tu..ana tatizo linaloitwa.."Yutongpolocummins..."
 
Back
Top Bottom