Sasa mbona kama mnachanganya madawa vile, maana mleta mada haeleweki nini kinamkuna kuna, anayumba sana. Mara anaongea mambo ya tarehe za uchapishwaji, mara kaibukia kwa hili la mikoa. Ingelikua bora aoge, apige meno mswaki halafu aje akiwa freshi na kuwa tayari kujadili na Wakenya.
Hizo headlines unazoziona hapo ni za hali ya juu sana na hazifanani na magazeti yenu ambayo yamejaa umbea tu, huwa hayana jipya zaidi ya taarifa za Diamond na Wema. Hauwezi ukapata udadavuaji wa Kikenya kwenye magazeti yenu. Niliyafuatilia sana wakati wa siasa za kampeni, jamani yalikua so unprofessional, yaliishia kuchukua misimamo na kuegemea kabisa bila aibu. Wengi iliwabidi mtegemee magazeti yenye waandishi Wakenya kama vile Citizen.
Haya hapa magazeti yenu