Hii inasikitisha, yaani kiwanda kikubwa kama hiki kinalipa Watanzania Tshs. 3800 kwa siku!

Wakuu ukoloni bado upo, hawa wahindi sio watu kabisa. Hivi kweli mfanyakazi anafanya kazi masaa 12 halafu unamlipa 3800 sasa hiyo pesa atafanyia nini.

Kwa kweli mtaani hali ni mbaya kama kweli tungekuwa uchumi wa kati hakuna mtanzania angeenda kufanya kazi kwa hao mashetani.

Cha kushangaza kampuni yenyewe ni kubwa (Sayona) huwezi hata ifikiria, kila siku inapigiwa promo/vinywaji na msanii mkubwa/Yuda

Serikali ya wanyonge iko wapi, hivi imeshindwa kuweka watu wa kumonitor na kuregulate mishahara ya wafanyakazi wasio rasmi. Kama ilivyoweka kwenye kitengo maalum cha kukusanya mapato.

Mishahara mizuri mizuri wanalipana wao na ndugu zao lakini ngozi nyeusi unakula 3800 na ukikaa hata siku moja utoro/ukiugua wanakukata mwisho wa mwezi.
We umegundua leo?Waziri mkuu alienda Urafiki akakuta mchina analipwa millioni 30,mbongo analipwa buku 2 kwa siku,Tena sio muajiriwa.
Serikali haiwezi kulazimisha kiwango Cha kulipwa,ikipiga kelele sana,watapunguzwa kibao,na kitaa kulivyo kugumu Bora uendelee kupokea hiyo hiyo buku tatu
 
Back
Top Bottom