Hii inasikitisha, yaani kiwanda kikubwa kama hiki kinalipa Watanzania Tshs. 3800 kwa siku!

Unataka walipwe shilingi ngapi?Unajua vigezo vinavotumika ili kupata hio bei ya 3800.Labda ni kupe mfano.Chupa moja ya soyana inaweza kuwa inauzwa TZS 500,Sasa ukianza kugawa gharama za uzalishaji wa chupa moja unapata kitu kinitwa unit cost.Sasa kwa kawaida kuna costs zinaitwa variable cost ambazo kimsingi ndizo ambazo mwekezaji anacheza nazo ili kupata faida.Zile fixed cost zinaweza kubadilishwa na innovation/teknolojia mpya.Kitu cha pili unapaswa kujua ni kwamba demand na supply ya labour(hao wafanyakazi inaendana na bei yao kama mko wengi mnaotaka kazi basi yule mwajiri anao uhuru wa kukulipa mshahara wowote anaotaka ukiona haufai unaondoka unamwachia kiwanda chake.

Kwa ufupi ni kwamba,watu wasome,waongeze skills,na waelewa haki zao kisha wakiona malipo ya kazi hayatoshi wanaacha tu mpaka mwajiri apandishe dau.Ukubwa au udogo wa kiwanda haundoi matumizi ya common sense.Mboa wewe unaweka hausigeli kwako unamlipa 50k na anafanya kazi 24hr hadi za mkeo anafanya lakini husemei hilo?Tuache unafiki na tukubali kwamba tatizo sio hao wahindi tatizo ni sisi wenyewe tunaotafuta kazi.
Kama serikali zingeruhusu waajiri watumie factors hizo bila kuingiliwa basi tungelipwa hata 25,000 kwa mwezi,na mishahara ingekuwa inabadilika kila siku,maana tajiri angeweza tu kusema kuwa mwezi huu gharama za uendeshaji zimeenda juu hivyo mishahara ipungue,ni lazima serikali iwepo katikati ili ku regulate,kuhakikisha kuwa kunakuwa na win-win situation baina ya mwajiri na mwajiriwa,mkapa aliwahi kufanya ujinga kama huo,akasema serikali isiingilie maslahi ya wafanyakazi wa mashirika na makampuni binafsi bali wao wenyewe wakae na kukubaliana kiwango cha malipo kwa mfanyakazi,hapo waajiri wakacheza na gap,watu walilipwa mishahara ya hovyo na hakuna pa kulalamikia,baadaye kikwete akajaribu kurekebisha hali,akatangaza kima cha chini cha mishahara,viwandani wakapangiwa walipwe 310,000 kwa mwezi,na alisema kabisa kuwa amekaa na chama cha waajiri,chama cha wafanyakazi,na bodies nyingine zinazohusika na kukubaliana kuwa kiwango hicho kinalipika! Baadaye kidogo waajiri wakapaa,wakarudi na kuiita serikali mezani,mwisho wa mchezo serikali ikatoka kapa,ikarudi kwenye mitambo na kututangazia kiwango kipya cha mishahara,ambacho ndiyo hiki anacholalamikia mtoa mada leo,magufuli anaogopa kuchokonoa mzinga wa nyuki,leo waajiri wana sababu elfu moja na moja za kwa nini wasipandishe mishahara,mzigo wa kodi,mazingira duni ya uwekezaji,natural disasters,unfair competition nk,hebu fikiria,leo serikali nayo imeingia ulingoni kupambana na wawekezaji wake ambao nao ni waajiri,serikali ambayo ndiyo mgambo,ndiye jaji,na ndiye hakimu,unategemea nini? Leo kampuni za ujenzi zinabaniwa kazi ili jkt ipenye kirahisi,benki binafsi zinaminywa p-umbu kisawasawa ili zile za serikali zi fly,ya fastjet si hekaya, mkuu,usitegemee serikali ya aina hiyo iwape nafasi nzuri wawekezaji ili wakose sababu za kuwakandamiza wafanyakazi wao,nchi imekuwa ya wachuuzi hii,mbele ya geti la kiwanda cha nguo kuna vibanda vya kuuza nguo toka china na hongkong,wamachinga wanalipa elfu 20 kwa mwaka kuuza bidhaa za china ambazo muhindi wa mlango wa pili ameajiri watanzania kibao kuzizalisha,utamwambia aongeze mishahara? Kodi kwanza
 
Serikali ilitunga sheria na kuweka minimum pay kwa kila sekta kuanzia wafanyakazi wajumbani 64000 kama hakai nyumbani, kama anakaa 40,000

Viwandani 3846 kwa siku

Sent from my TECNO W2 using JamiiForums mobile app
Sasa mbona lawama zinaenda kwa muhindi,kumbe ni baba yetu mwenyewe ndiye aliyeamuru tulipwe hiyo peanut?
 
Mimi wangu simtesi..nikijiskia kutoka out niko naye ....kifup mm nakula bata na beki 3 wangu vby mno tu..amerelax...analala kuliko mm..na sina shaka naye na wala sion kwro..usik analala saa6 anachek mamichezo...anafanyaje kaz kwa 18hrs?
Ndo maana nikasema msaidizi WA nyumbani akiwa hateswi na boss wake anajali changamoto zake, mbona wanakipato ambacho ni fairly. Kuna wengine mpaka wanawaendeleza zaidi, sasa sijajua hapo utumwa unakujaje kwa nijibu wa Andoza.
 
Na hao mnaowaambia waandamane, waelimisheni wapate vibali kutoka jeshi la polisi kwanza.

Sawa mkuu???
Siku watakayoenda kuomba hicho kibali ndiyo siku watakayoanza kuujua uchungu wa rungu kwenye goti!! Hata wakipewa hicho kibali siku ya maandamano hutamwona hata mmoja barabarani,wote watakuwa nyumbani na mabandeji magotini,"acha tu niwaambie ukweri"
 
Maajabu ni kwamba vibarua wao wa kihindi hawalipwi ela iyo....
Wakati flani akaletwa kijana wa kihindi nimfundishe kazi,siku naiona salary slip yake nikachanganyikiwa kabisa,analipwa kama milioni saba za bongo na mimi nalipwa 1.3 kabla ya makato,na hapo haikuwa tanzania hii,ilikuwa ghana,hii shida haipo kwetu tu.
 
Bora niuze karanga au mihogo mibichi au miwa nina uwezo wakupata

huo mshahara hata na zaidi,wengi wa wafanyakazi wa huko Akili zao zime stuck

yani kama ni saa basi imeisha betri inahtaji replacement ya betri jipya,ila hamna kazi

ngumu kama kazi za viwandani tena viwanda vya wahindi,oh yooo yooo yooo yooo kheee
 
Right to self determination.Huyo unakaa naye kama ndugu yako na sio kama mfanyakazi wako.Fanya hivi,Mkatia Bima ya Afya kwa ajili yake na dependants wake.Mlipe Salary isiopungua 180k,mpe chakula kila siku 5000 itakuwa ni 150k kwa mwezi ndo mshahara wake utafika 450k ambayo bado kuna wanalipwa that amount na wanaona ni ndogo sana.Usichanganye kazi na kumhifadhi mtu kama mtumwa wako kisha ukamhudumia vizuri ili awe comfortable na kuendelea kuwa mtumwa wako.
Mimi sina uwezo huo mkuu nna watoto 2 wakubwa wanaojiosha...sina kazi kwangu hata ya kumtoa mtu jasho zaid ya uwepo wake home...naona unahemkwaa..ova mie naibu waziri😏
 
Ndo maana nikasema msaidizi WA nyumbani akiwa hateswi na boss wake anajali changamoto zake, mbona wanakipato ambacho ni fairly. Kuna wengine mpaka wanawaendeleza zaidi, sasa sijajua hapo utumwa unakujaje kwa nijibu wa Andoza.
Angalia alichoniambia nifanye..ahaha yaan amefikisha kama 450k🤣mshahara wa mtu mwenye degree kbs...
 
Mkuu hawa vibarua ambao kupata kwao kibarua ni kuwahi kufika na kwa mwezi anaweza pata kibarua mara 6 vibarua ambao hata miezi mitatu hawafikishi!!
Mkuu ukiacha kazi sehemu nyingi si unapata kazi mahala pengine utatumia namba ile ile ya uchangiaji NSSF mimi nakuambia sasa, vibarua wengi hata kwenye fao la matibabu linawaokoa sana shib, hata barmaid wanatakiwa wachangiwe nssf usiwe mbishi nakueleza kitu nachokijua
 
Mimi sina uwezo huo mkuu nna watoto 2 wakubwa wanaojiosha...sina kazi kwangu hata ya kumtoa mtu jasho zaid ya uwepo wake home...naona unahemkwaa..ova mie naibu waziri😏
Hapana,sio wewe wala sio personal,nazungumzia tu FACT kuhusu kazi za ndani kwa ujumla wake.Tena nafikiri wewe unaweza kuwa unajitahidi ila kuna wengine wanaweza kuwa hata kale kamshahara kadogo wanawarusha.Its pathetic.
 
Serikali ndiyo ya kulaumiwa kwani kama kungukuwa na mazingira wezeshi hakuna mtu angefanya huo upuuzi lakini niwakumbushe kuwa huko mtaani hali ni mbaya Sana nijuavyo hiyo kampuni inayolipa 3800 hata wakishusha hadi 1000/day badi watu watajazana.

Hii nchi ni kama koloni la mtu tena Bora angekuwa mzungu sasa ni mtu mweusi wanaume wazima na familia zao wiki inakatika hajaweka buku akipata kazi hapo sayona hata akilipwa 1000 atashukuru kwa kupata mahala pakutuliza akili cha ajabu ikitokea kampuni likasema linataka watu wa ku volunteer bado watajazana.
Unadhani ingekuwa kweli tupo uchumi wa kati wangetuchezea hivi?
 
Wakuu ukoloni bado upo, hawa wahindi sio watu kabisa. Hivi kweli mfanyakazi anafanya kazi masaa 12 halafu unamlipa 3800 sasa hiyo pesa atafanyia nini.

Kwa kweli mtaani hali ni mbaya kama kweli tungekuwa uchumi wa kati hakuna mtanzania angeenda kufanya kazi kwa hao mashetani.

Cha kushangaza kampuni yenyewe ni kubwa (Sayona) huwezi hata ifikiria, kila siku inapigiwa promo/vinywaji na msanii mkubwa/Yuda

Serikali ya wanyonge iko wapi, hivi imeshindwa kuweka watu wa kumonitor na kuregulate mishahara ya wafanyakazi wasio rasmi. Kama ilivyoweka kwenye kitengo maalum cha kukusanya mapato.

Mishahara mizuri mizuri wanalipana wao na ndugu zao lakini ngozi nyeusi unakula 3800 na ukikaa hata siku moja utoro/ukiugua wanakukata mwisho wa mwezi.
Msiwe wepesi kulaumu je mmejiuliza wana make faida kiasi gani kwenye serikali hii ya kusingizia madeni ya miaka 47 ya kodi,kulundikiana kodi,kupeana makadilio mengingi ya kodi na tozo mbalimbali.
 
Ndio maana huwa nawashangaa mnaoshadidia viwanda kama njia ya ajira,hao vibarua hata kodi hawalipi faida ya viwanda ni kuongeza thamani ya bidhaa sio ajira kama wengi wanavyodhani
 
Back
Top Bottom