Hii inamaanisha nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii inamaanisha nini?

Discussion in 'JF Doctor' started by Invisible, Nov 15, 2008.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Nov 15, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Kwenu madaktari,

  Kwa muda wa majuma takribani mawili ama matatu (hadi leo) watu wengi (I may say more than 60%) jijini Dar es Salaam wanaumwa aidha mafua ama vichwa ama wanajihisi malaria ama miili kuchoka sana.

  Nimewasiliana na watu si pungufu ya 20 ni mmoja tu aliyenifahamisha kuwa yeye mzima (bukheri wa afya).

  Sasa: Kama wataalam wa masuala ya afya, nini tatizo haswa? Mabadiliko ya hali ya hewa? (Najua huu ni msimu mzuri kwenu... :) )

  Nasubiri kwa hamu kujua nini haswa tatizo!
   
 2. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Hali ya hewa itakuwa imechangia. Mgandamizo wa hewa (pressure & humid)?

  Mi nimeanza kujisikia vyema sasa.
  .
   
 3. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #3
  Nov 15, 2008
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Mimi sijaona tofauti yoyte katika afya yangu siku za karibunni. Lakini kama mtu yeyote afya yake ni mbaya ajihadhari na mbu wasimng'ate,avute hewa safi,anywe maji safi, halafu amuombe Maanani,ameeze anasumbuliwa na nini,imeanza lini,ainasababishwa na nini,na zipo sympton zipi.
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Nov 15, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mimi si daktari, ila Kwa ufahamu wangu, wale wanao ishi nchi za baridi zenye kufata kalenda ya summer, winter nk, kipindi hiki ni kipindi cha kupata chanjo za mambukizo ya flu I thinks kuanzia Sept ili kupata kinga ya flu kipindi cha winter.
  Wakazi wengi wa nchi za ulaya na Amerika wanapatiwa chanjo za kuzuiya hii flu kipindi hiki.

  Kila msimu una matatizo na maradhi yake, sisi tunaoishi nchi maskini tunashindwa tu kufahamishwa na serikali zetu kwa sababu za kukosa wataalam, au kwa sababu zisizo wezekana. Labda kwa kukosa wataalam wa kujuwa haya mambo na mabadiliko ya hali ya hewa na madiliko ya kimwili pamoja na maambukizo ya maradhi mbali mbali.

  Nakumbuka moja ya research ilikuwa inaangalia kwa nini kipindi cha majira ya joto kuna kuwa na jinai 'crime' nyingi kushinda majira mengine. Result zinasema kuwa binadamu mara nyingi huwa na hasira anapokuwa katika hali ya joto na anashindwa kufikiria kwa makini, matokeo yake yanakuwa ni ugomvi husio na lazima. Sawa sawa na mtu aliyekosa usingizi kwa kipindi cha siku mbili tatu.

  ______________________________________________________________
  FYI: Polisi na watu wa intelligence, wanatumia mbinu hizi za kuwahoji wahalifu kwenye chumba chenye joto au kukukosesha usingizi kabla ya kuwahoji.
  Wanachofanya aidha Watakuhoji kwenye chumba chenye joto au baridi. Au kukunyima usingizi kwa siku mbili tatu kabla ya kukuhoji, mbinu hizi hutumika tu pale wanaposhindwa kupata taharifa wanazo zitaka kutoka kwa wahalifu kwa njia ya kawaida.
  .

  _______________________________________________________________

  Kwa hali iliyoko hivi sasa ni matokeo ya msimu wa hali za hewa tu.
  Kwa ushauri zaidi unachotakiwa kufanya ni kumuona mtaalam (psychologist) au daktari aliye karibu nawe pale unapoona mabadilliko yasio ya kawaida katika afya zetu, tabia na matendo yetu.

  X-Paster
   
Loading...