IzukeneJr
JF-Expert Member
- Aug 4, 2012
- 758
- 753
Wakati flani nikiwa chuoni miaka kadhaa nyuma, nilikuwa nimekaa na jamaa yangu tukipiga story mbili tatu juu ya mahusiano. Katika mengi aliyoyaongea kuna sentensi moja huwa naikumbuka mpaka leo. Jamaa aliniambia, “Ebana kwakweli mimi hata Mungu ni shahidi yangu, nimejitahidi sana kutii amri zote za Mungu lakini ki ukweli hii moja ya kuzini ishanishinda…”
Nilimuuliza kwanini anasema hiyo dhambi imemshinda, na katika majibu yake alielezea ugumu anaokutana nao kuepuka vishawishi vya wanawake wazuri na warembo anaokutana nao kila siku na ukizingatia yeye ni kijana mtanashati ambae wanawake wengi wanavutiwa kuwa naye.Pia akaelezea mazingira yanayomzunguka (chuoni) ambapo alisema ni mazingira mabayo hata ukijitahidi kukwepa hivyo vishawishi kwa kiasi gani inakuwa ngumu sana na mwisho unajikuta umeangukiamo.
Hiyo ilikuwa miaka kadhaa iliyopita lakini leo naliongelea hili maana naamini ni watu wengi sana wanaiamini hiyo sentensi hapo juu.Wanaamini kwamba haiwezekani kuiepuka dhambi ya uzinzi maishani mwao.Na imefikia mahali sasa uzinzi umekuwa ni kitu cha kawaida kufaywa na hata watu hawaionei haya tena.
Ninalo neno kwa ajili yako unaesoma ujumbe huu, Ukweli utabaki kuwa ukweli hata kama utaukimbia au kujifanya hujausikia au kuuficha kwa namna yoyote ile, ukweli utabaki kuwa ukweli tu. Na ukweli wa jambo hili ni kwamba, Zinaa ni njia ya mauti na mwisho wa hayo yote utahukumiwa kwa kufanya zinaa. Vitabu vyote vya dini vimeandika hivyo na imani zote zinaasa hivyo.
Je ni kweli kwamba huwezi kuikwepa zinaa? Hapana sio kweli, hayo ni maneno tu ya kuhalalisha unachofanya. Maandiko yanasema hakuna jaribu lililo nje ya uwezo wako, umepewa mamlaka ya kuuamrisha mwili wako ufanye lolote unalotaka ulifanye. Ukiuamrisha mwili wako kwa kuuambia, “Mwili tulia” unatakiwa kukutii. Uzinzi ni matokeo ya tama na hisia za mwili. Tatizo kubwa la tulio wengi tumeruhusu tamaa zetu ndo zitawale maamuzi yetu, hilo ni kosa kubwa.
Wewe ni mkubwa sana kuzidi hisia na tamaa za mwili wako. Jitahidi sana mara zote mchana na usiku mwili wako uwe chini ya control ya maamuzi yako, na siyo maamuzi yako kuwa chini ya control ya hisia zako. Muombe Mungu muda wote akusaidie kufanya maamuzi kwa muongozo wake. Yes you can do it, unaweza kuzishinda tamaa na ukakwepa dhambi ya uzinzi maana Mungu amekupa huo uwezo ndani yako. Usiitetee dhambi, haina huruma hiyo itakupeleka motoni.
Mungu akubariki sana
#SeeYouAtTheTop
Share
Fabian Izukene

miendo yao wanavyotembea na huyo bata anavyotikishwa hatareee.