Hapa tutakuwa tunatupia mambo yanayokera katika jamii,kama vile tabia zikerazo,vijimambo na issues nyingine zikerazo,lengo ni kuwazindua wahusika "Acheni hizo"
Zinikerazo mie
1. Mama ntilie kumfuta mwanae kamasi kwa mkono-kavu halaf kuendelea kuwahudumia wateja bila kunawa.INAKERA
2. Jamaa katoka 'kuchimba viazi' na ulimwona hakunawa,halafu anakupa mkono kukusalimia.INAKERA
3. Unakuta kidume hakijishughulishi na kazi yoyote,halafu mishe zake ni "Oya ntoe buku nkapone".INAKERA
Endelea kutupia zingine.