Hii imetokea juzi huko Segerea

cyberspace

JF-Expert Member
Jul 23, 2011
724
286
Askari polisi wawili cpl James na Bahati wa kituo cha Stakishari walikutana na jamaa mmoja amebeba jeneza, wakajua hii ni deal huyu jamaa anapeleka wapi jeneza hili kukuu itakua ameiba hivyo lazima wamtoe kitu kidogo la sivyo lazima wamtie korokoroni.

Askari hao walimsimamisha jamaa ambapo aliitika wito na kusimama kama kawaida ya polisi walianza makeke ya kumtisha jamaa kwa maswali lukuki.

Jamaa hakuonekana kutishika akawaeleza hili jeneza la sanduku mnaloliona ni la kwangu, ndugu zangu wamenizika sehemu ambayo sikuipenda sasa naenda kujizika sehemu ambayo ni nzuri, basi naombeni twende mnisaidie kunizika.

Wakati wanashangaa wanashindwa cha kujibu yule jamaa akatoweka machoni mwao. Walitaharuki na kuanza kukimbia mpaka Cpl. Bahati akavunjika mguu sasa amelazwa muhimbili.
 

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
704
Kweli askari wanapenda rushwa, ni ugonjwa kwao. Iko siku watapoka rushwa toka kwa Shetani mwenyewe! Watakiona kiama!
 

Konya

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
921
114
Si angewatoa tu na chochote maanake hawa jamaa bila mlungula maisha hayaendi,au ni moja kati ya mafunzo wanayopata wakiwa depo?
 

KISABENGO

Member
Sep 23, 2011
18
2
Ahahahahaaaaaaaaa humu ndani kuna watu wanamatatizo ya kisaikolojia wao mda wote wanataka uzungumze siasa,umseme rais yaan'hii inachekesha sanaaa tu'
 
4 Reactions
Reply
Top Bottom