Siku hizi hakuna mwanamke wa peke yako.
Unaweza shangaa demu unaemuona wako peke yako anakuchukulia wewe ni mchepuko maana ana bwana 'ake anaemchukulia wake peke yake.
Kuna jamaa alikuwa ana demu, akahisi ni mke mtarajiwa kabisa jinsi walivyopenda.
Demu alikuwa ana mtu anaemtumia pesa na mahitaji yote, kaseviwa uncle kwenye simu. Na jamaa kaambiwa uncle ndie anaemsomesha na kumlipia hostel. Na huyo uncle ni kaka wa mama yake demu.
Siku moja jamaa kazuka hostel kwa demu bila taarifa anakuta uncle nae yupo kapeleka mahitaji (hakuwahi kumuona kabla, zaidi ya kusikia akitajwa tu).
Cha ajabu jamaa anamuona mzee wake; kumbe uncle ni baba mzazi wa jamaa kwa maana sugar daddy (uncle) wa demu ni baba mzazi wa mshkaji.
Jamaa katoswa na demu akawa mama yake wa kambo.