Hii Imekaaje Wataalamu!

Hii Imekaaje Wataalamu!

Ryzen

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
7,312
Reaction score
8,754
Kipindi cha Nyuma Mama yangu Hakuwahi kabisa kupenda niwe na mahusiano au Mazoea na Mwanamke yeyote, alitaka nisome nifikie Malengo yangu...Kwa Hili Niliona Yupo sahihi!.

Basi nikamaliza Mpaka Form six bado Mama akawa Hapendezwi na mimi kuwa na uhusiano wowote japo mzee hata akipata hizo story Hana Noma utamsikia tu bwana kuwa Makini usiharibu Malengo yako.

Kwa ideology hio nikawa nshajenga picha kwamba mama yangu hapendi niwe na uhusiano na wanawake maana utamsikia kwambaa mara wanawake wana siri nyingi usijione unapendwa, wengine ni mashetani wanakuja kwa dizaini hio kukuharibia Malengo.

Sasa Bwana cha Ajabu, Juzi kati watu wa pembeni walimfikishia taarifa kwamba nadate na binti mmoja hivi....kama kawaida nikajua mama atamind (Namheshimu sana mama na sipendi kabisa akwazike).

Mama akaniuliza Mwanangu Nasikia uko na binti fulani (sura yake ikionesha furaha ambayo nahisi hakuitaka niitambue), nikamwambia ndio ni kweli mama (kwa aibu nilimjibu ivo), kwa kawaida nilijua angemind lakini nashangaa mama hakumind akaniambia kuwa makini yule binti si ndo yupo form six? nikamjibu ndio.

Akarudia Sikuambii ummwache mwanamke wako ila kuwa Makini (Jambo ambalo huwa si kawaida kwa mama), sasa after that mama katokea sana kumpenda uyu binti, kidogo nikifanya ujinga ananitania labdaaooh fulani angejua upo hiivii....n.k.

sasa wadau hii imekaaje sometimes nashindwa kuelewa au mama ananichora? maana binti ambae nampenda the most nae anampenda na anaonesha kila dalili angetaman siku moja nimuweke ndani uyu mtoto.

Je nijipe amani au nachorwa? Maana si kawaida ya Mama navomjua.
 
Kwanza nianze kwa kumpongeza mama yako
Mama yako anafahamu kijana Kama wewe huna experience yoyote juu ya mahusiano Sasa anachohofia huenda ukajisahau kabisa na kupotelea kwenye dimbwi la mapenzi na badae kujikuta hata mama yako akikwambia Jambo humsikilizi, lakini Mara nyingi aina hii ya wazazi huwa wanawapenda Sana watoto wao na unakuta ni huyo mmoja ndio kamuweka kipaumbele.
 
Mama ni mzazi na mlezi wa maisha yetu, anatambua kuwa umekua kiasi cha mwili wako kuwa na matamanio ya uhitaji wa mwenza wako lakini vilevile kwa factor hiyo hiyo ya kukua kwako mama anakubaliana na mawazo yako kwamba sasa unahitaji kuanza kujifunza namna ya kuishi na mwenza wako kwa akili
 
Kwanza nianze kwa kumpongeza mama yako
Mama yako anafahamu kijana Kama wewe huna experience yoyote juu ya mahusiano Sasa anachohofia huenda ukajisahau kabisa na kupotelea kwenye dimbwi la mapenzi na badae kujikuta hata mama yako akikwambia Jambo humsikilizi, lakini Mara nyingi aina hii ya wazazi huwa wanawapenda Sana watoto wao na unakuta ni huyo mmoja ndio kamuweka kipaumbele.
Umeongea Fact maana am first born na Mama amekuwa akinipenda kuliko ata wengine!
 
Yap anaelewa anachokifanya kwa sababu nguzo ya wenzako wanao fuata na njia ni wewe mtoto wa kwanza inabidi awe imara ya asiharibu malengo yake, kuwa makini maana mtoto wa kwanza kiroho ananguvu na mara nyingi shetani huwa anapenda sana kuharibu na kuvuruga watoto wa kwanza.
 
Mmh subiri umuweke mimba mapenzi yata ongezeka zaidi
 
Utoto bhana. Sasa hapo unaxhoshindwa kujua kama mama amekuchagulia mchumba ni nini?
 
amechoka kukukataza kaona huelewi kichwa kigumu.. kaona akupe support sasa ufurahi na roho yako halafu utajua baadae alikuwa anamaanisha nini..!!!
 
Yap anaelewa anachokifanya kwa sababu nguzo ya wenzako wanao fuata na njia ni wewe mtoto wa kwanza inabidi awe imara ya asiharibu malengo yake, kuwa makini maana mtoto wa kwanza kiroho ananguvu na mara nyingi shetani huwa anapenda sana kuharibu na kuvuruga watoto wa kwanza.
Amen, Kiongozi Umeongea Ukwelii! Hii Elimu Natamani kuijua vizuri!
 
Mama Mama Mams Maamaaa mamaaaa....

Mxyy..
 
I thought shule zilifunguliwa this week! Au dogo langu alinipiga changa la macho ili avute mkwanja nn?
 
Kipindi cha Nyuma Mama yangu Hakuwahi kabisa kupenda niwe na mahusiano au Mazoea na Mwanamke yeyote, alitaka nisome nifikie Malengo yangu...Kwa Hili Niliona Yupo sahihi!.

Basi nikamaliza Mpaka Form six bado Mama akawa Hapendezwi na mimi kuwa na uhusiano wowote japo mzee hata akipata hizo story Hana Noma utamsikia tu bwana kuwa Makini usiharibu Malengo yako.

Kwa ideology hio nikawa nshajenga picha kwamba mama yangu hapendi niwe na uhusiano na wanawake maana utamsikia kwambaa mara wanawake wana siri nyingi usijione unapendwa, wengine ni mashetani wanakuja kwa dizaini hio kukuharibia Malengo.

Sasa Bwana cha Ajabu, Juzi kati watu wa pembeni walimfikishia taarifa kwamba nadate na binti mmoja hivi....kama kawaida nikajua mama atamind (Namheshimu sana mama na sipendi kabisa akwazike).

Mama akaniuliza Mwanangu Nasikia uko na binti fulani (sura yake ikionesha furaha ambayo nahisi hakuitaka niitambue), nikamwambia ndio ni kweli mama (kwa aibu nilimjibu ivo), kwa kawaida nilijua angemind lakini nashangaa mama hakumind akaniambia kuwa makini yule binti si ndo yupo form six? nikamjibu ndio.

Akarudia Sikuambii ummwache mwanamke wako ila kuwa Makini (Jambo ambalo huwa si kawaida kwa mama), sasa after that mama katokea sana kumpenda uyu binti, kidogo nikifanya ujinga ananitania labdaaooh fulani angejua upo hiivii....n.k.

sasa wadau hii imekaaje sometimes nashindwa kuelewa au mama ananichora? maana binti ambae nampenda the most nae anampenda na anaonesha kila dalili angetaman siku moja nimuweke ndani uyu mtoto.

Je nijipe amani au nachorwa? Maana si kawaida ya Mama navomjua.
Soma kijana wanawake wapo tu huku mjin bila kuwa na grisi ya kutosha hutoweza kufanakisha yote hayo
Wanawake wapo tu tena wako weng sana kata kitabu,soma kama umekunywa maji ya bendera
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom