Hii imekaaje wakuu....

gasgas

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2015
Posts
1,098
Reaction score
994
Habari za jioni mabibi na mabwana.

Nimeona niilete hii kwenu pia nisikie mnasemaje.

Mimi ni kijana wa kiume miaka 25. Kuna mdada nilitokea kumpenda sana kutokana na uzuri wake, tabia na ukarimu wake. Moyo wangu ulidondokea hapo.

Nilimtoa date moja na tulienjoy sana, kwenye maongezi yetu, body language, tulikuwa tunaendana vizuri. Na ilikuwa kila siku lazima tuwasiliane kwa text messages kila siku, kila wakati.

Ikafika wakati nikamchombeza naye akakubali bila shida tuwe wapenzi kwa kuwa hata yeye alinikubali.

Tukaanza mahusiano rasmi kama wapenzi.

Kadri siku zilivyokuwa zinakwenda naanza kuona mambo yanakuwa tofauti. Naanza kuhisi kama kuna vitu mwenzangu anazidisha mno mpaka inaanza kuwa kero kwangu.

Mimi ni mtu mmoja mpole, mtaratibu, sipendi mambo mengi, an introvert. I like to have some breathing space. Napenda maisha yangu ya kawaida yaendelee.

Ila yeye akaanza kuwa clingy and needy. Atapiga simu siku nzima bila kujali nipo kazini, au nipo barabarani. Na usually nikipokea huwa hamna cha kuongea since siku nzima tumeshinda tukiwasiliana kwenye text message so nafahamu siku yake imeendaje na anafahamu kila kinachoendelea kwangu.

Ilifika kipindi anapiga simu tunasalimiana, halafu anakaa kimya kwa nusu dakika mpaka inabidi nimshtue tena halafu tunaagana.

Baada ya nusu saa anapiga tena na story ni ile ile. Na ana namna ya kuongea kwenye simu ambayo ni ngumu kumwelewa anachoongea, sijui ndio mapozi lakini inabidi utumie nguvu za ziada kumwelewa anachoongea kwenye simu

Outing zetu za hapo mwanzo zilikuwa nzuri sana na nilikuwa naenjoy company yake kichizi. Ila kadri siku zinavyokwenda naona hali inabadilika.

Tunaenda sehemu nzuri, tunaspend 4 hours pamoja tukienjoy. Hapo mimi naona imetosha tuondoke lakini yeye atang'ang'ania tuendelee kubaki hapo for 4 more hours, bila sababu maalumu.

Hakuna tunachofanya na unakuta amechoka sana na usingizi umemshika, basi atajilaza hapo kwenye kifua changu, lakini hataki kwenda nyumbani ukifikiria i am already tired of mazingira hayo.

Shida kubwa ni hii contrast in personality.
I love the girl, but i feel suffocated na nimemwambia more than once, anasema ameelewa lakini haionyeshi katika maongezi na matendo yake.

Analalamika nikiangalia mpira, analalamika nikicancel appointment yetu ili kufanya issue ya maana inayohusu kazi zangu,

Imefikia kipindi anapiga simu naiona inaita lakini sipokei au natafuta namna ya kucancel appointment zetu.

Kuna wakati nilitaka kumwacha lakini ananipenda mno na yupo desperate. Na hata mimi nampenda lakini vitu anavyofanya vinanifanya nipoteze interest taratibu.
 
Mkuu, sisi wanaume huwa tunapuuzia maudhi madogo kama hayo ili kuyafanya mahusiano yetu yawe yenye afya.
Na hivyo ndivyo mwanamke anae kupenda kwa dhati huwa. Na kuna wakati atakupigia hata sim na kisha atakosa la maana kukueleza.
Kwangu mimi nakushauri tu kwamba mpende huyo binti, maana hapo hajui kama anakukwaza. Pia jaribu tu kuwa mvumilivu kwasababu hayo ni maumbile yao hawa wwnzetu.
 
Connection imeshapota...ulimpendea nini kama kero zake huzipendi.
 
Mapenzi yameshawashinda ninyi, tafuteni ustaarabu mwingine...as long as ninyi si mume na mke
 
nAuNgA mKoNo hOjA
 
She is the first person i contact and the last before i go to sleep.

I tell her all my secrets, my fears and all there is.

Kuna vitu labda kutokana na personality yangu vinanizidi
Let love aside, huna interest nae tena.

If you can't be her friend....stop being her lover ASAP!!
 
Umenipa mtazamo tofauti kidogo.
Nashukuru mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…