Hii imekaaje wakuu

Akili ya midume kabla ya kuoa,

Mke asipomjali na kumpenda mama yangu kwakweli itabidi tu tuachane, yaani mama yangu alivyonihangaikia kwakweli sitaki mtu wa kumnyanyasa kabisa, ikitokea nikaoa mwanamke asiyempenda na kumjali mama yangu basi hata mimi hawezi kunipenda na kunijali pia, mama ndio kila kitu bwana, ameuza mpaka mkaa ili tu niweze kwenda shule.

Baada ya kuoa sasa halafu bahati mbaya kaoa mke asiyemjali mama yake.

aaaah! huyu mama bwana ni msumbufu sana, yeye anapaswa kuishi na huyu mke wangu kwa akili la sivyo mimi sintaweza kujenga familia, yeye anapaswa kumuelewa huyu mke wangu kuwa akili zake ziko resi sana, aaah! yaani mama amekuwa kikwanzo katika ndoa yetu, yaani mama hajaliwi tena hapo, kila kizuri ni kwa mke tu mama hakumbukwi tena, kanga mpya haijui mpaka ccm wampe baada ya miaka mitano.

Wakuu tuwajali sana mama zetu kwa hali na mali tusijisahau, wadada pia mnapoolewa jitahidi sana kuwajali hawa wamama, wengine wamebaki wajane kwa hiyo mume alobakia wa kumjali na kumhudumia ni mume wako hivyo muwe na huruma sana.

Nawasilisha.
daah nimechelewa hata kuoa nmmalizie nyumba yake,gari nlishamnunulia tayari nadhan ntakayemuoa akikuta mama yangu anajiweza itakua ngumu kumletea dharau za kipuuzi au nakosea jamani!
 
Kweli kabisa kama una mpenda mama yako unashindwaje.kumpenda mama wa mwenzio??

Tena mama yako aweza kuwa na vitimbi zaidi ya mama mkwe wako
 
daah nimechelewa hata kuoa nmmalizie nyumba yake,gari nlishamnunulia tayari nadhan ntakayemuoa akikuta mama yangu anajiweza itakua ngumu kumletea dharau za kipuuzi au nakosea jamani!
Mkuu huna ulilokosea hapo, kubwa umuonyeshee upendo wa dhati km mama.
 
Kwanza hakuna kama mama,na huwezi kumpenda Mama yako mzazi ukashindwa kumpenda mama wa mwenzio,na kama unaweza kumstahmilia mama yako mzazi na huenda akawa na vitimbi kuliko mama mkwe,hata mama mkwe awe mkorofi vipi
wewe ukimuonyesha ukarimu wallah atabadilika na nafsi yake itamsuta....
Hivyo ndio inavyotakiwa, sasa unakuta mwingine anashindana na mama mkwe mpaka inafikia hatua ya kurushiana maneno,huko si kujichumia laana.
 
Akili ya midume kabla ya kuoa,

Mke asipomjali na kumpenda mama yangu kwakweli itabidi tu tuachane, yaani mama yangu alivyonihangaikia kwakweli sitaki mtu wa kumnyanyasa kabisa, ikitokea nikaoa mwanamke asiyempenda na kumjali mama yangu basi hata mimi hawezi kunipenda na kunijali pia, mama ndio kila kitu bwana, ameuza mpaka mkaa ili tu niweze kwenda shule.

Baada ya kuoa sasa halafu bahati mbaya kaoa mke asiyemjali mama yake.

aaaah! huyu mama bwana ni msumbufu sana, yeye anapaswa kuishi na huyu mke wangu kwa akili la sivyo mimi sintaweza kujenga familia, yeye anapaswa kumuelewa huyu mke wangu kuwa akili zake ziko resi sana, aaah! yaani mama amekuwa kikwanzo katika ndoa yetu, yaani mama hajaliwi tena hapo, kila kizuri ni kwa mke tu mama hakumbukwi tena, kanga mpya haijui mpaka ccm wampe baada ya miaka mitano.

Wakuu tuwajali sana mama zetu kwa hali na mali tusijisahau, wadada pia mnapoolewa jitahidi sana kuwajali hawa wamama, wengine wamebaki wajane kwa hiyo mume alobakia wa kumjali na kumhudumia ni mume wako hivyo muwe na huruma sana.

Nawasilisha.
Naamini nafasi ya mama ni ile ile. Not even the wife comes before the Mom.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom