Kakole
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 2,094
- 1,745
Akili ya midume kabla ya kuoa,
Mke asipomjali na kumpenda mama yangu kwakweli itabidi tu tuachane, yaani mama yangu alivyonihangaikia kwakweli sitaki mtu wa kumnyanyasa kabisa, ikitokea nikaoa mwanamke asiyempenda na kumjali mama yangu basi hata mimi hawezi kunipenda na kunijali pia, mama ndio kila kitu bwana, ameuza mpaka mkaa ili tu niweze kwenda shule.
Baada ya kuoa sasa halafu bahati mbaya kaoa mke asiyemjali mama yake.
aaaah! huyu mama bwana ni msumbufu sana, yeye anapaswa kuishi na huyu mke wangu kwa akili la sivyo mimi sintaweza kujenga familia, yeye anapaswa kumuelewa huyu mke wangu kuwa akili zake ziko resi sana, aaah! yaani mama amekuwa kikwanzo katika ndoa yetu, yaani mama hajaliwi tena hapo, kila kizuri ni kwa mke tu mama hakumbukwi tena, kanga mpya haijui mpaka ccm wampe baada ya miaka mitano.
Wakuu tuwajali sana mama zetu kwa hali na mali tusijisahau, wadada pia mnapoolewa jitahidi sana kuwajali hawa wamama, wengine wamebaki wajane kwa hiyo mume alobakia wa kumjali na kumhudumia ni mume wako hivyo muwe na huruma sana.
Nawasilisha.