Hii imekaaje ndugu zangu?

Hii imekaaje ndugu zangu?

Bishweko

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
4,280
Reaction score
2,980
Wanajamvi,

Kuna jambo limenitokea maishani na sikutegemea. Nilimpata mdada wa Kihehe tukaanza safari ya maisha na tukapata mtoto wa kiume kwa sasa ana miezi kuna mmoja. Wiki kama tatu hizi atuishi wote maana siku natoka kazini nilikuta kaondoka na mtoto na mfanyakazi.

Nikawa napiga simu hapokei, baada ya mda nikaambiwa kuwa yupo kwa dada yake . Sasa nikipiga simu anapokea shemeji yake ambaye anamuoa dada yake nakuniambia eti sijalipa mahali. Sasa najiuliza mahali inabidi nidaiwe na mtu ambaye tumeoa familia moja au ndo utamaduni wa wahehe na kwanini huyu jamaa ndo anapokea simu hiyo.

Nitafunguka zaidi wanajamvi, lakini nipeni ushauri lipi la kufanya
 
Wewe nunua mbwa au kamata mbwa koko mpelekee huyo mhehe kisha atakupa mkeo
 
Kama maongezi kwa njia ya simu hayajakusaidia;nenda uonane nao, muongee ana kwa ana.
 
Unatafuta Suluhu kwa Simu ?????????

Naona kama ulimchoka vile ??????

Hebu Chukua Hatua kiutu uzima
 
Kaongee na mkeo then uende kwa wazazi wake umalize hilo swala kaka acha poteza mda
 
Shemegi anataka kuzima taa tu huyo hana jengine

Mkuu yaani nashtuka maana niliwai ona sms za ajabu kutoka kwa jamaa kwenye simu ya mke wangu. Sasa kwenda nitaenda lkn huyu jamaa simuelewi kabisa
 
Ushauri gani? we toa mahari urudishiwe mke baas
 
Bora kashtuka manake ulikua unasubiria akuzalie wa pili then umwambie yeye siyo wife material
 
Funga safari, ukifika tafta mw/kiti wa mtaa then uende kwa huyo jamaa akueleze kwann kaamua kuondoka na mkeo wakati yy sio mzazi wake.
 
Peleka washenga kwa wazee wa huyo binti, katoe mahari na fanya haraka uoe. Wameona labda hueleweki, mpaka unamzalisha ndugu yao bado upo kimya. Usije ukafikisha watoto watatu alafu ukamtosa ndugu yao.
 
Ni hivi km huyo kaoa dadake na dadake ni mkubwa kwenye familia basi huwa wana mamlaka hayo km wazazi wamemuarifu afanye kutokana na umbali au uzoefu wa kukabiliana na ww. Hiyo nikukubana wewe mwizi wa binti yao. So wako sahihi kwa tamaduni za huko. Kalipe mahari utakaaje na mtoto wa mwenzio unamtumia bila ghalama...
 
cha kufanya hapo usijifanye kichwa ngumu kuwa upande wa waliokosea na uende na kama hiyo mahari unayo ilipe japo nina imani kuna lingine waliloliona hilo la mahari ni kelele tu...
 
Wanajamvi,

Kuna jambo limenitokea maishani na sikutegemea. Nilimpata mdada wa Kihehe tukaanza safari ya maisha na tukapata mtoto wa kiume kwa sasa ana miezi kuna mmoja. Wiki kama tatu hizi atuishi wote maana siku natoka kazini nilikuta kaondoka na mtoto na mfanyakazi.

Nikawa napiga simu hapokei, baada ya mda nikaambiwa kuwa yupo kwa dada yake . Sasa nikipiga simu anapokea shemeji yake ambaye anamuoa dada yake nakuniambia eti sijalipa mahali. Sasa najiuliza mahali inabidi nidaiwe na mtu ambaye tumeoa familia moja au ndo utamaduni wa wahehe na kwanini huyu jamaa ndo anapokea simu hiyo.

Nitafunguka zaidi wanajamvi, lakini nipeni ushauri lipi la kufanya

Kwani shemeji mtu kasema umpelekee yeye? Tumia akili, unakaa na mtoto wa watu bila mahali akikufia wahehe watakudai mahali msibani ukiwa umefiwa na mwanamke ndo unamuoa.
 
Mkuu yaani nashtuka maana niliwai ona sms za ajabu kutoka kwa jamaa kwenye simu ya mke wangu. Sasa kwenda nitaenda lkn huyu jamaa simuelewi kabisa

kwanini hukusema tangu mwanzo???? kalipe mahari huko
 
Kwahiyo kama mtu ujatoa mahari kwa wahehe mtu ambaye amekutangulia kuoa kwenye familia anaweza kumchukua mkeo daaaah

hajamchukua wamepanga wote na dada na ndugu na wazazi upeleke mahari uoe!!!
 
Hii ni changamoto kweli maana kwetu mke akitoka kwako bila kuaga inabidi uachane naye.Lakini nakubali mahari nitalipa ya kumzarisha tu nasi kumuoa maana uwezekano wa kuwa jamaa aliwai kumega na bado anamega
 
Back
Top Bottom