Hii imekaa visuri. Uchovu wa kisiasa wa kikewte na wapambe waki!

Mboja

Senior Member
Sep 29, 2010
157
23
KAULI za Rais Jakaya Kikwete, Waziri wake, Steven Wassira na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, John Chiligati, Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, wapambe wake Augustine Mrema (TLP), John Cheyo (UDP) na Anne Kilango (CCM) dhidi ya maandamano na mikutano ya CHADEMA imedhihirisha uchovu wa kisiasa unaowakabili.
Wote pamoja wamejigeuza kikundi cha sanaa za kisiasa kinachoimba tenzi za watawala dhidi ya wananchi. Uzoefu wao umegeuka ukale usioendana na usasa wa siasa za Tanzania.
Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi uliopita, Rais Kikwete alilalama kinyonge kwamba maandamano ya CHADEMA yanatishia amani na yanalenga kuiondoa serikali yake madarakani; akaomba wananchi wawapuuze wanasiasa hao wa upinzani.
Wananchi wakampuuza. Wameendelea kuomba CHADEMA iandae maandamano na mikutano mingine katika maeneo yao. Kati ya maandamano na mikutano yote iliyofanyika Kanda ya Ziwa, nimeshuhudia miwili.
Wananchi wanaandamana kwa hiari yao. Hawalazimishwi. Hawanuni. Hawatishani. Hawapigani. Hawakanyagani. Wanaimba nyimbo “za harakati.”
Wanasikiliza hotuba za viongozi kwa utulivu wa hali ya juu. Inapobidi wanashangilia au wanapiga makofi.
Kwa vitendo hivi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA wamedhihirisha mambo mawili. La kwanza ni amani. Wanaandamana kwa amani, na wanahudhuria mikutano yao kwa amani.
Kwa maana hiyo, mikutano ya CHADEMA haihatarishi amani. Kama kuna amani iko hatarini kwa sababu ya mikutano hiyo, ni amani ya watawala. Amani ya wananchi inalindwa na wananchi wenyewe.
La pili ni majibu yao kwa Rais Kikwete. Hawakuhitaji kumjibu kwa maneno bali kwa vitendo.
Na hili linatufikirisha na kutueleza kwamba amani ya wananchi inakuwa hatarini pale ambapo vyombo vya dola vinaingilia maandamano na mikutano ya wananchi.
Imetokea Arusha. Maandamano yalianza kwa amani. Polisi walipoingilia, kwa msukumo wa kisiasa, ndipo vurugu zikatokea. Hata siku ya mazishi ya mashujaa waliouawa, ambayo kimsingi ndiyo ingekuwa na shari, ilikuwa ya amani na utulivu kwa sababu moja tu – polisi hawakujihusisha na maandamano hayo.
Katika maandamano ya Mwanza, Musoma, Shinyanga na Bukoba, polisi hawakuvuruga maandamano na mikutano ya CHADEMA. Yalifanyika kwa amani.
Kwa mantiki hii, wananchi wamekejeli vitisho vya Rais Kikwete. Na watu wote wenye akili timamu, wanajua kuwa hofu ya JK inatokana na ukweli kwamba ‘amekataliwa na wananchi.’
Rais wa nchi aliyechaguliwa kihalali na anayeamini kwamba anaungwa mkono na wananchi, hawezi kuwa na sababu ya kuonyesha hofu kama hii iliyodhihirishwa na Kikwete.
Anachokiogopa, na kinachosababisha woga wake anakijua mwenyewe. Kiongozi jasiri halalami. Anapaswa kutoa hotuba yenye kuonyesha mamlaka inayolingana na nafasi yake. Hii ya JK ilikuwa hotuba dhaifu.
Kwa bahati mbaya, Wassira, Tendwa, Chiligati, Kilango, Mrema na Cheyo wamejiingiza katika kuimba hofu ya Rais Kikwete. Wakajidhalilisha.
Wassira anasema: “CHADEMA wanaandamana kueneza chuki…wameshindwa kwa njia ya kidemokrasia, wanataka kutumia nguvu …tunachotaka ni amani. Ni wazi CHADEMA wanaonyesha wao ni washari, wanawatia wananchi hofu. Kama wana hoja wasubiri kikao cha Bunge.” :mullet:
 
Back
Top Bottom