Unakumbuka kesi ya Zombe- mauaji ya wafanyabiashara wa madini, 2002?
Hata hapa majuzi hujasikia kesi ya kubambikiza huko Mtwara, ikapelelea mauaji, hadi Mama akaingilia? Unafikiri hizo ni kesi za kisiasa?
Sio polisi wote ni waadilifu, wengine vibaka pia. Miaka kadhaa imepita, kule Mvomero, Polisi walimuwekea mfanyabiashara fuvu la binadamu na kumuundia kesi ili atoe rushwa. Hapo unasemaje?