Hii hapa Dawa ya Panya Road

Hata kama mkuu, kwani hao wanaokamatwa kwa kuzushiwa ndo huwa wanaachiwa baadae? Tena hao ndo huwa haieleweki hata wameishia wapi. Mtaskia tu kapigwa risasi ya mguu akafa wakati anajaribu kukimbia, au kaugua hadi kufa akiwa mahabusu.
 
Mna akili za kikatili sana. Halafu mnadhubutu kwenda makanisani na misikitini kusali na kuswali.

Tanzania imesaini mikataba ya haki za binadamu. Kila binadamu hata aliyevunja sheria, ana haki ya kusikilizwa na kuadhibiwa kwa namna sheria zinavyosema.

Tukitaka kutenda matendo ya kinyama kama hayo, tuwaite al-shabaab waje watutawale. Au sisi wenyewe tujitangaze kuwa tumeweka sheria pembeni kwa muda ili tuuvae unyama na kutenda hayo mambo ya kinyama.

Ushauri wangu ni serikali kuongeza nguvu, ubunifu na weledi wa jeshi la polisi. Kama ikiwezekana hili jeshi la nchi nzima lipunguzwe ukubwa ili yaundwe majeshi madogo madogo ya majiji, miji nk. yanayoendana na mahitaji ya mahali husika.

Tusikubali jeshi la polisi lijifiche na kukimbia jukumu la ulinzi na usalama wa raia na mali zao. Tusikubali kujiingiza kwenye umwagaji damu usiofuata misingi ya sheria.
 
Wanapelekwa sehemu ya wazi ya umma mfano Pale Mwembe yanga wanapandishwa juu ya kama stage waandishi wa habari na wananchi wakishuhudia wanamiminiwa risasi za moto,then wanashushwa na kwenda kuzikwa na jiji...hiyo ni kimya kimya hakuna kuongea.....
Unasema waandishi wa habari na wananchi washuhudie, halafu unakuja kusema tena ifanyike kimya kimya! Nadhani haujatulia kiakili
 
Unachosema huwa kinafanyika...husikiagi "Jambazi hilo lilipigwa risasi lilipojaribu kuwatoroka polisi wakati likipelekwa kuonesha lilipoficha silaha na wenzake...."


Hapo jambazi ashaminywa, kawataja wenzake wote, maficho yote ya silaha na zimeshapatikana..matukio yote yaliyopiga kisha baada ya hapo ni paa! Paa! Paa! Then press conference JAMBAZI LILIUAWA LILIPOJARIBU KUTOROKA
 
Mkuu mwanza mitaa ya kwetu vibaka wote waliacha na wengine waliuwawa na wengine kuhama magazine na kukimbia kusikojulikana.

inasemekana kulikua na msako wa vibaka kimya kimya ukikamatwa unapelekwa kigoto unapigwa risas unaenda zikwa na jiji.. kuna watu nawafahamu kama watatu ni vibaka walipotea mpaka leo haijulikani walipo.

inasemekana walikamatwa wakapigwa risas na askar mpaka sasa huku kitaa hali ni shwari vibaka wote walishahama.. hao waliopotea mpaka leo haijulikan na gerezan hawapo kiufup hiyo opereshen imeleta amani mitaa yetu
 
Sasa wewe una uhakika gani kwamba wote wamehusika na hilo tukio

Kama wamehusika na ushahidi upo nini maana ya kuundwa sheria na mahakama

Unashawishi watu wachukue sheria mkononi wakati unajua ni kinyume Cha sheria
 
Hakun cha kujiskia wala kujiona. Ukikamata panya road, peleka mwembe yanga mwagia petrol piga moto wote.
 
Wakipatikana panya road ni kupiga na kuchoma Moto mpaka waishe. Yaani ni tairi tu
 
Haki za kimataifa za nyokwe, hao waliotunga hizo sheria wenyewe wanauwa watu tena wasio na hatia sembuse mwizi red-handed, China is my best country when it comes to deal with stupid issues .
 
Wahalifu ujulikana maana huwa ni kundi sasa kama mmewatawanya mkawakamata wachache waliokuwa kwenye group utasemaje sio wahalifu
Uhalifu ukifanyika, polisi wanakuwa na pressure ya kukamata wahalifu na kuonesha jamii kuwa jeshi la polisi lipo na linalinda raia. Katika pressure hiyo, huwa mara nyingine wanabambikiza watu wasiohusika. Inaweza isiwe hivyo mara zote, lakini haya mambo yapo.
 
Hakuna mkuu dawa ya hawa watu ni kuwamaliza tu hautasikia ujinga tena
Hivi wewe kuna unyama zaidi ya watu mob kukuvunjia nyumba wakaingia ndani ukajeruhiwa wewe mkeo na watoto kubakwa mbele yako na wanaondoka na mali bado unatetea unyama huo?
Kweli watanzania nyerere alitutoa nyongo
 
Hayajakukuta wewe
 
Hebuwaelezee hawa wengine humu wanaoleta siasa kwenye kutafuta amani..
 
Sasa wewe una uhakika gani kwamba wote wamehusika na hilo tukio

Kama wamehusika na ushahidi upo nini maana ya kuundwa sheria na mahakama

Unashawishi watu wachukue sheria mkononi wakati unajua ni kinyume Cha sheria
Kuna yule askari wa magereza juzi kati hapa aliyeenda mbeya kwao akamuua baba yake wazi wazitena mbele ya mama mzazi pale unataka uchunguzi wa nini?
 
Hawa vijana wanastahili adhabu Kali sana ambayo siifahamu,maana hawa NDIYO majambazi ya kesho!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka km chizi yaan
Mkuu ujue sijaandika kwa mihemko, ni swal ambalo liko moyoni mwangu muda mrefu.
Nikiwa raisi polisi nitawachapa sana fimbo. Yani hhhiii!!!!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka km chizi yaan

Swala lingine ni swala la kodi, nikiwa raisi (day dreaming) nitapunguza kodi zote za kila aina to the lowest minimum,ila kila mtu LAZIMA ALIPE KODI.

Nikitaka kwenda ziara ya eneo fulani, natanguliza wapelelezi , nikikuta kuna watu hawalipi kodi, meneja tra wa eneo hilo atavuta pumzi ya moto
 
Sheria kali inaweza ikawekwa, lakini tusisahau pia namna polisi wanavyobambikia watu makosa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…