Hii hali TANESCO haivumiliki

Hii hali TANESCO haivumiliki

Mlendamboga

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2011
Posts
668
Reaction score
347
Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo utaratibu wa kurejesha mgao wa umeme kiaina, hali imeendelea kuwa mbaya siku hadi siku.Jana ofisi za serikali hasa zenye kutumia kompyuta zile zisizokuwa na standby generator imekuwa shida. Leo tena tangu saa 12 jioni gizani mwendo mdundo hii nini? Nazungumzia mkoa wa Mbeya, sijui mikoa mingine
 
Arusha, Mwanza, Shinyanga, Kahama, Mwanza na Geita hakuna umeme. Pia watu wa Dar nao wanalalamika. Mgao wa umeme umerudi wanaona aibu kutangaza maana Profesa Kikwete aliahidi mgao wa umeme kuwa historia
 
Morogor Mjini... Hali ni hiyo hiyo. Tena mbaya zaidi toka asubuhi saa kumi na mbili umeme unakata na kurudi kila dakika mbili....hatari sana kwa vifaa vyetu vya gharama.... Mda huu umekatika moja kwa moja...
 
Nimepata taarifa kutoka kwa mfanyakazi wa Tanesco ilala na amedhibitisha huu ni mgao usio rasmi mpaka tupige kelele ndio utangazwe hii ndio tanzania
 
Arusha, Mwanza, Shinyanga, Kahama, Mwanza na Geita hakuna umeme. Pia watu wa Dar nao wanalalamika. Mgao wa umeme umerudi wanaona aibu kutangaza maana Profesa Kikwete aliahidi mgao wa umeme kuwa historia
na prof. muhungo alijinasib pia. aliahidi kwa mbwembwe huku akiwakejeli 'watu' ya kuwa hakutakuwa na mgao. hivi yupo wapi siku hizi? au 'keshatulizwa'? Lizaboni, MSALANI, ifweero, MwanaDiwani tujulisheni! dar kuanzia last week umeme unakatika hata kwa saa 12. hii nchi imekuwa kama jehanum, mateso sana. tanesco na washirika wenu #BringBackOurMoney
 
Last edited by a moderator:
mmh hii ni hatari .....lkn ndo tz yetu mwendo wa giza na majoto haya sasa.....
 
Kuna kila sababu ya kukipiga hiki chama cha majangili chini lkn sijui tumelogwa! Hivi ni nani anawapaga hawa mbwa mwitu kura! Shenzi sana ccm..
 
Kibaha umeme ulikatika juzi saa 10 jioni ukarudi jana saa 11 jioni, leo saa 5 asbh umekatika na bado haujarudi na haijulikani kama utarudi au ndo niagieni tenaa!
 
Nipo Kitunda huku hamna umeme tangu asubuhi...
 
Kwetu Ifakara alhambdulilah kwa jina la yesu kristo kukatika kweli Ni nAdra.ndo hivyo 100% ya watzia Watu wazmaaaa tumelogwa chapachapa
 
Eff word TANESCO. Moja ya kero zangu ni tanesco na foleni hapa Dar, nilikuwa kwenye comp nafanya kazi yangu, umeme umekatika kama masaa 2 hivi. Sijui niwatukanaje hawa fisi!
 
hv kwanini kila kipindi cha joto kikianza na mgao nao unaanza? ni kwamba mashine zao huwa zinapata moto sana zinashindwa kufanya kazi au?
 
Jamani nilidhani kwetu tu,nipo mbweni umeme ulikatika toka jana saa moja jioni wakaurudisha usiku nadhani kwenye mida ya saa saba au nane usiku,haya na leo asubuhi ndio imekuwa kamchezo unakatika na kurudi ht siwaelewi hawa tanesco.
 
Nimepata taarifa kutoka kwa mfanyakazi wa Tanesco ilala na amedhibitisha huu ni mgao usio rasmi mpaka tupige kelele ndio utangazwe hii ndio tanzania

Nani apige kelele? Watanzania zinapokuja issues serious kama hizi hata Uzi unaohusu mgao wa umeme ukiwekwa humu haupati wachangiaji wakati kuna athari za moja kwa moja kwenye makusanyo TRA. We angalia ukiwekwa Uzi wa Diamond na Wema wachangiaji wake then linganisha na Uzi wa mgao wa umeme. Huu umaskini sio Mungu katuonea, ni halali yetu. Profesa Kikwete yupo anapiga misele dunia nzima
 
Njoeni kahama ndo muone mgao wa ukweli..huku hatushangai umeme kukatika ila tunashangaa umeme ukirudi...maana tushazoea daily lazima wakate,jana wamekata samoja jioni mpaka leo mchana bado haujarudi kudadadeki...
 
Kimara mwisho toka asubuhi ya saa kumi na moja hakuna umeme.
 
Back
Top Bottom