Wakuu natumaini mtakuwa salama kuna hali fulani huwa siielewe , Mimi ni kijana Wa kiume Nina rafiki zangu Wa kike huwa napenda kuwatembelea Mara kwa Mara hasa kipindi cha wikiendi au mud a nikitoka kazini , nawasalimia tunaongea ila nikikosa cha kuongea naaga na kuondoka zangu huwa sipendi kuwaboa kukaa nao muda mrefu Sana bila kuongea naweza nikakaa hata mwezi Kama sina cha kuongea nakaa tu nyumban , muda mwingi huwa nalifikiria ili swala nakosa jibu nahisi Kama najitenga na jamii kwakutoonesha ushirikiano nao napenda sana kusocialize na watu ila nashindwa kwa sababu ya hii hali ,wakuu naomba mnisaidie nifanye nin kuepukana na hii hali