Hii chapati niliyotengeneza, usipokua makini utajing'ata Vidole

Mtu akiolewa na mwanaume anejua kupika ndio anakuwa makini balaa, na anafit sana jikoni kwani anajua akifanya vitu ovyo mumewe anaelewa. Sasa mtu alieolewa na mume asiejua kitu Chakula kiunguzwe, kipikwe ovyo kisiwive vizuri ye anaona sawa tu, tena anaogoa hata kusema ukweli anaogopa asije akaambiwa apike yeye kama anaweza. Lakini anaejua haoni tabu kukosoa anajua hata akiambiwa pika mwenyewe anaweza
Uweeeeee habar ya kukosoana mapish nan kasema,bas bora akosoe kimahaba mahaba,unkuta linanuna na chakula linazira pumbaaaafu
 
Hizo ni chapati za maji?
Nakushauri ingia youtube utakutana na mwanamama Aroma kila aina ya pishi utalikuta kwake, ni vema kuangalia na kufanya kuliko kusoma.

Me pia mapishi mengi nimejifunzia youtube.

Turudi kwa topic yetu, chapati za maji, weka yai/mayai, vitunguu maji, karoti na hoho au kimoja wapo katika hivyo ili kuleta ladha na kukata ile harufu ya yai.

Mchanganyiko wako usiwe mzito sana wala mwepesi sana, size ya kati. hapo utatoa kitu mwake mwake, mafuta weka kiasi sio kama unakomoa, unapakaza tu juu ya chapati sio unamwagia.
Unafanyaje mchanganyiko uwe mwepesi au mgumu?
 
Back
Top Bottom