Hii Bongo HAKUNAGA

Ona tena anavyochemka kwa mara nyingine...natamani anielewe lakini ndugu yangu huyu anazidi kunifanya nicheke teh! teh!...

Huyu atakuwa ameshashiba urojo wa pemba!!teh teh teh teh!ni vema tuachane naye,sisi tujikite kwenye mjadala wetu!
 
Mkuu usiwe unabisha tu...ungejaribu walau kuuliza wala watu8 asingepata ugumu kukujibu...
Wachawi huwa wanawanga usiku kwa kuwa huwa kumetulia nadhani umeshindwa tu kuunganisha dots hakuna adanganyaye hapa...
Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu, uliposema usiku kumetulia hata wanaJF wamekunukuu, sasa unakataa unabadilika na kuhamia kwenye hoja ya ulozi.
Jipange...

Mkuu Amavubi alianza hivi...angalia kuna neno usiku hapo.
Hufanyika mto Pangani lakini nyakati za usiku tu.......

Halafu akafuatia Mkuu Kimanzichana kutaka kujua kwa nini hufanyika usiku tu na si wakati mwingine.
Mkuu kwanini nyakati za usiku tu?

watu8 said:
Kwa kuwa hali ya hewa inakua imetulia tuliiii...
Hili ndio likawa jibu langu kwa Kimanzichana kwa kuwa naifahamu Pangani kwa mambo ya ULOZI na moja kwa moja nikawa nimeielewa post ya awali ya Amavubi.


Hii ndio maana ya kuwa GREAT THINKER, huitaji kuandikiwa notes kama nifanyavyo kwako!!! unanimalizia WINO wangu wa KEYBOARD UJUE :becky::becky::glasses-nerdy::glasses-nerdy:
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…