Hii bahati ni ya kawaida au ya namna gani wakuu?

Midazolam

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
806
1,337
Moja kwa Moja kwenye mada.mimi ni mkristo na muumini mzuri tu katika maisha yangu.

Nimekuwa na hii hali na imekuwa inajirudia sana ninapokuwa msafi wa rohoni na huwa ninapoomba sana.

Nimekuwa nikienda kununua kitu dukani basi nitatoa ela na kununua bidhaa,ila Cha ajabu nitarudishiwa ela nyingi au juu zaidi,

Mfano juzi nilienda kunyoa nywele saluni nikatoa elfu kumi nikampa kinyozi nikamwambia kata elfu nne yako ,kinyozi akanirudishia elfu kumi na mbili nikamwambia aisee mbona umenirudishia kibao,nikachukua elfu sita nikamrudishia Ile ela yake iliyozidi

Jioni nikaenda dukani kunununua maji Huwa nachukua kwa dazani kwa ajili ya kuweka ndani,akaniambia jumla unatakiwa kulipa kumi na mbili na mia mbili nikampa elfu 20,Cha ajabu amenirudishia tena kama elfu kumi na nane.nikamwambia dada umenizidishia ela,akashukuru sana ,kwenye hiyo duka ni kama mara mbili ,akasema aisee kaka una roho nzuri mdogo wangu pia aliwahi kukuzidishia ela ila kwa uaminifu wako ulimrudishia nikamwambia sitaki kula ela ambayo si jasho langu.

Huku kazini siku iliyofuata nikaenda kununua chakula Cha elfu tatu maeneo ya hapa hapa kazini,yule kaka naye akajichanganya akanirudishia tena ela iliyozidi nilimpa elfu Tano akanirudishia elfu nane ,kwa kweli hii sikurudisha Mungu anisamehee,

Swali nafanya vizuri kurudisha hizi ela au makosa ? Wajuzi wa haya mambo nisaidieni nijue.

Nb hii hali hata nikipanda daladala nimekuwa na bahati ya kutoombwa ela na konda ,atanipita tu kama hanioni vile ila Kuna mda nafsi inanisuta nachukua ela na kulipa.
 
Hayo mambo huwa yanatokea Sana mkuu

Kubwa ujue dhuluma ni mbaya,kwahiyo unachofanya ni sahihi kabisa,hata konda akisahau kukudai ujue kutomlipa kwako ni dhuluma pia Ile ni biashara kama nyingine Tu.
 
Niliwahi kusema Mimi siku moja Mungu atanizawadia watoto watatu,mke wangu na huo ujauzito tumboni na namuomba Mungu atawabariki na kuzaliwa.nimekuwa pia na hiyo kawaida na kuwaambia wajawazito kuwa tumboni una mtoto wa kiume au wa kike,akizaliwa ni vile vile najikuta tu natamka,Kuna Moja pia nilimtamkia mapacha alivyoenda kupima mimba ya miezi mitatu ultrasound ikasoma kweli anapacha alifurahi yule mama sijapata kuona, inanitokea tu najikuta natamka,na sijaowahi kukosea.na ni wengi sana hapa ndo nilianza kujihisi
 
Unafanya vyema kabisa mkuu, kuna watu wakizidishiwa chenji wanaona halali yao. Huo ndio ucha Mungu
 
Huku kazini siku iliyofuata nikaenda kununua chakula Cha elfu tatu maeneo ya hapa hapa kazini,yule kaka naye akajichanganya akanirudishia tena ela iliyozidi nilimpa elfu Tano akanirudishia elfu nane ,kwa kweli hii sikurudisha Mungu anisamehee,
Umrudishie haraka huyu anayehangaika na maisha halafu unamdhulumu haki yake. Huo ni wizi wa dhahiri kabisa kwani unajua alikosea hesabu na bado ulinyamaza.

Na unakuja kujisifu kuwa ni mtu msafi wa kanisa!
 
Soma mpaka mwisho uelewe,nilizungumza nn hapo au nilitampa nn hapo.
 
Moja kwa Moja kwenye mada.mimi ni mkristo na muumini mzuri tu katika maisha yangu.

Nimekuwa na hii hali na imekuwa inajirudia sana ninapokuwa msafi wa rohoni na huwa ninapoomba sana.

Nimekuwa nikienda kununua kitu dukani basi nitatoa ela na kununua bidhaa,ila Cha ajabu nitarudishiwa ela nyingi au juu zaidi,

Mfano juzi nilienda kunyoa nywele saluni nikatoa elfu kumi nikampa kinyozi nikamwambia kata elfu nne yako ,kinyozi akanirudishia elfu kumi na mbili nikamwambia aisee mbona umenirudishia kibao,nikachukua elfu sita nikamrudishia Ile ela yake iliyozidi

Jioni nikaenda dukani kunununua maji Huwa nachukua kwa dazani kwa ajili ya kuweka ndani,akaniambia jumla unatakiwa kulipa kumi na mbili na mia mbili nikampa elfu 20,Cha ajabu amenirudishia tena kama elfu kumi na nane.nikamwambia dada umenizidishia ela,akashukuru sana ,kwenye hiyo duka ni kama mara mbili ,akasema aisee kaka una roho nzuri mdogo wangu pia aliwahi kukuzidishia ela ila kwa uaminifu wako ulimrudishia nikamwambia sitaki kula ela ambayo si jasho langu.

Huku kazini siku iliyofuata nikaenda kununua chakula Cha elfu tatu maeneo ya hapa hapa kazini,yule kaka naye akajichanganya akanirudishia tena ela iliyozidi nilimpa elfu Tano akanirudishia elfu nane ,kwa kweli hii sikurudisha Mungu anisamehee,

Swali nafanya vizuri kurudisha hizi ela au makosa ? Wajuzi wa haya mambo nisaidieni nijue.

Nb hii hali hata nikipanda daladala nimekuwa na bahati ya kutoombwa ela na konda ,atanipita tu kama hanioni vile ila Kuna mda nafsi inanisuta nachukua ela na kulipa.
hili tangazo ulipie kwa Max wa JF..
 
Back
Top Bottom