eti nini? uongo wa Mwenyekiti wa Kamati, uongo wa serikali? Huyu kweli Kidato cha nne, hiyo hoja isngezuia bunge kuahrishwa kwa vile angetakiwa kuleta ushahidi wa uongo wa LUKUVI, PINDI CHANA na AG, jambo ambalo nina uhakika hakuwa na ushahidi huo na yeye ni muongo, MBOWE anataka kutuambia kuwa ni uongo kwamba hawakupeleka majina ya LISSU na BAREGU kwa Rais?
Huwa nashangaa sana akili ndogo inaongoza akili kubwa.
Watu kama Dr.Kitilia.
Prof. Baregu, Zitto, Prof.Safari, na wengine wengi wote wapo chini ya Mbowe,
Ndiyo maana unaona watu kama Sugu ndiyo watetezi wake.
kama hiyo ndo hoja ya Mbowe, hakika ameonesha ujinga wa hali ya juu au inaelekea alikuwa anawaza mengine bungeni. Mbunge wa CUF alitoa hoja ya kuomba mjadala wa Rasimu ya Katiba uahirishwe. Naibu spika akahoji wanaoafiki na wasio afiki. wasio afiki walishinda ila CHADEMA hawakukubali. John Mnyika akaomba kura zihesabiwe. ndipo kila mbunge akahojiwa. waliounga hoja ya mbunge wa CUF walikuwa 59 tu na walioikataa walikuwa 156. kabla ya matokeo kutangazwa Naibu Spika alitahadhalisha kuwa hataruhusu hoja nyingine baada ya matokeo
Ndiyo, imesajiliwa Tanzania. Tofauti ni kwamba mkataba wa usajili wa meli ya kinana unatoa fursa kwa meli hiyo kusafirisha meno ya tembo, bangi nk hadi pale CCM itakapofikia ukomo wa kutawala nchi.Meli ya Kinana iliyobeba meno ya Tembo nayo imesajiliwa Tanzania kama ile ya Bangi ya Italia?
Wewe ndie msemaji mkuu wa huyo kiongozi?
Kwanza, nilichotaka kusema ni kutoa hoja ya kuomba shughuli za Bunge zisitishwe kwa muda ili Kamati ya Uongozi ya Bunge ijadili makandokando yote ambayo yalikuwa yametokea juu ya muswada huo, ukiwamo uongo wa mwenyekiti wa kamati ya Bunge, uongo wa serikali bungeni na masuala mengine yote, ili sasa Bunge lipate mwelekeo chanya juu ya muswada huo na mchakato mzima wa Katiba Mpya kwa masilahi ya wananchi.
Hivyo hoja yangu ilikuwa muhimu sana kusikilizwa, ili viongozi wakutane kuokoa jahazi na kuondoa sintofahamu ambayo hatimaye imesababisha mjadala mkubwa na muswada mbovu kupitishwa bungeni kwa masilahi ya upande mmoja wa CCM, Mbowe alikaririwa akisema.
yeye mwenyewe machokumchuzi anasemaje? au wewe ndiye msemaji wake?
Nashukuru kwamba unatambua kwamba Tanzania Daima ni kisima cha habari, isipokuwa sasa wameanza kupoteza. Walianza Uhuru/Mzalendo/Habari Leo, wakaja Mtanzania/Rai, wamekuja TBC na sasa yanaelekea kuwakumba Tanzania Daima. Lakini kwa Tanzania Daima nafikili ni kwa sababu ya matunda yake hivyo wanweza endelea na mfumo huo kwani mti wenye matunda ndiyo urushiwao mawe.Lazima litakuwa Tanzania Daima, hiki kigazeti siku hizi ni michosho ile mbaya, Tangu KIBANDA aondoke huko limekuwa kama jarida na siyo gazeti tena.
Labda wewe ndo mjinga kama Ndugai!Kwa hiyo hii hoja ilimjia baada tu ya kura kupigwa? Kwa nini alishauri kura zipigwe huku akijua muswada ni mbovu? Kwa uelewa wake anadhani watanzania wote ni wajinga kiasi kwamba kila anachoongea yeye basi ni lulu? Kama Mbowe anadhani kujitambua ni kuishabikia Chadema na kukubali kila kisemwacho na kifanywacho na viongozi wake basi amekosea sana. Uzalendo wa taifa umetuingia kuliko uzalendo wa kichama.
Tuwe waangalifu:
Suala ni je: alilotaka kusema Mbowe ndilo hilo? Mtoa thread athibitishe
Na je: ilikuwa sahihi kwa Ndugai kumkataza Mbowe kusema lolote, hata kama si hilo linalodaiwa na JME?
eti nini? uongo wa Mwenyekiti wa Kamati, uongo wa serikali? Huyu kweli Kidato cha nne, hiyo hoja isngezuia bunge kuahrishwa kwa vile angetakiwa kuleta ushahidi wa uongo wa LUKUVI, PINDI CHANA na AG, jambo ambalo nina uhakika hakuwa na ushahidi huo na yeye ni muongo, MBOWE anataka kutuambia kuwa ni uongo kwamba hawakupeleka majina ya LISSU na BAREGU kwa Rais?
Kama hicho ndiyo alikuwa anataka kukisema Mbowe basi atakuwa ana mapungufu mengi katika masuala ya kibunge.
Mbowe, anatakiwa kujua kuwa bunge linaendeshwa kwa utaratibu wa sheria na kanuni za kibunge, siyo kila anachosema watu wakubali kuna utaratibu wa kupiga kura kama alivyoomba mbunge mwenzake Mnyika, kura zikapigwa kwa mujibu wa demokrasia wengi wakashinda.
Chadema wanataka kulazimisha maoni yao ndiyo yawe kauli za watanzania.
Labda wewe ndo mjinga kama Ndugai!