Hichi ndicho Mbowe alikusudia kusema

jme

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2013
Posts
4,782
Reaction score
5,172
“Kwanza, nilichotaka kusema ni kutoa hoja ya kuomba shughuli za Bunge zisitishwe kwa muda ili Kamati ya Uongozi ya Bunge ijadili makandokando yote ambayo yalikuwa yametokea juu ya muswada huo, ukiwamo uongo wa mwenyekiti wa kamati ya Bunge, uongo wa serikali bungeni na masuala mengine yote, ili sasa Bunge lipate mwelekeo chanya juu ya muswada huo na mchakato mzima wa Katiba Mpya kwa masilahi ya wananchi.
“Hivyo hoja yangu ilikuwa muhimu sana kusikilizwa, ili viongozi wakutane kuokoa jahazi na kuondoa sintofahamu ambayo hatimaye imesababisha mjadala mkubwa na muswada mbovu kupitishwa bungeni kwa masilahi ya upande mmoja wa CCM,” Mbowe alikaririwa akisema.
 

Kwa hiyo walikuwa anawapotea watu muda kukubali kura zipigwe?
 

eti nini? uongo wa Mwenyekiti wa Kamati, uongo wa serikali? Huyu kweli Kidato cha nne, hiyo hoja isngezuia bunge kuahrishwa kwa vile angetakiwa kuleta ushahidi wa uongo wa LUKUVI, PINDI CHANA na AG, jambo ambalo nina uhakika hakuwa na ushahidi huo na yeye ni muongo, MBOWE anataka kutuambia kuwa ni uongo kwamba hawakupeleka majina ya LISSU na BAREGU kwa Rais?
 
Hivi kumbe uamuzi wa kura unaweza kupingwa kwa njia hiyo pia? kweli demokrasia ina sarakasi nyingi sana.
 
chanzo cha habari tafadhari

Lazima litakuwa Tanzania Daima, hiki kigazeti siku hizi ni michosho ile mbaya, Tangu KIBANDA aondoke huko limekuwa kama jarida na siyo gazeti tena.
 

kama hiyo ndo hoja ya Mbowe, hakika ameonesha ujinga wa hali ya juu au inaelekea alikuwa anawaza mengine bungeni. Mbunge wa CUF alitoa hoja ya kuomba mjadala wa Rasimu ya Katiba uahirishwe. Naibu spika akahoji wanaoafiki na wasio afiki. wasio afiki walishinda ila CHADEMA hawakukubali. John Mnyika akaomba kura zihesabiwe. ndipo kila mbunge akahojiwa. waliounga hoja ya mbunge wa CUF walikuwa 59 tu na walioikataa walikuwa 156. kabla ya matokeo kutangazwa Naibu Spika alitahadhalisha kuwa hataruhusu hoja nyingine baada ya matokeo
 
Hivi kumbe uamuzi wa kura unaweza kupingwa kwa njia hiyo pia? kweli demokrasia ina sarakasi nyingi sana.

Mkuu tatizo elimu, inawezekana hata hakujua kwa nini kura zilikuwa zinapigwa.
 
Lazima litakuwa Tanzania
Daima, hiki kigazeti siku hizi ni michosho ile mbaya, Tangu KIBANDA
aondoke huko limekuwa kama jarida na siyo gazeti tena.

mkuu, wengi wanaolinunua si kwa lengo la kusoma bali kufungia maandazi na kujipungia upepo kwa wale wanaoishi sehemu zenye joto bila ya kuwa na vipoza joto
 

Wewe tulikuwa pamoja kumbe katika kufuatilia sakata zima tangu mwanzo, haujakosea hata nukta mkuu.
 
Mkuu tatizo elimu, inawezekana hata hakujua kwa nini kura zilikuwa zinapigwa.

Tehetehetehe. haya ndo madhara ya akili ndogo kuongoza akili kubwa. Lissu anajitahidi sana kumtetea lakini anaonekana anatwanga maji kwenye kinu. nina hakika hata yale yaliyoandikwa na msemaji wa kambi ya upinzani ambayo kwa kiazi kikubwa yameidhalilisha CHADEMA ni kutokana na hoja za Mbowe. hivi form four unategemea nini
 
Naona magamba leo mmeambiwa mtalipwa buku 8 mmekunywa chai lakini?
 
Kama hicho ndiyo alikuwa anataka kukisema Mbowe basi atakuwa ana mapungufu mengi katika masuala ya kibunge.

Mbowe, anatakiwa kujua kuwa bunge linaendeshwa kwa utaratibu wa sheria na kanuni za kibunge, siyo kila anachosema watu wakubali kuna utaratibu wa kupiga kura kama alivyoomba mbunge mwenzake Mnyika, kura zikapigwa kwa mujibu wa demokrasia wengi wakashinda.

Chadema wanataka kulazimisha maoni yao ndiyo yawe kauli za watanzania.
 
source tanzania daima
 
hakika CHADEMA wanazidi kujidhalilisha
Huwa nashangaa sana akili ndogo inaongoza akili kubwa.

Watu kama Dr.Kitilia.
Prof. Baregu, Zitto, Prof.Safari, na wengine wengi wote wapo chini ya Mbowe,

Ndiyo maana unaona watu kama Sugu ndiyo watetezi wake.
 

Ndungai na maccm waliyo kuwepo siku hiyo walifanya ujinga wa hali ya juu sana kwa kushindwa kusikiliza ujinga wa mwenzao ili wautolee maamzi.ndugai na ccm yake walivyo choka na kujaa ujinga hawana hata uwezo wa kujibu ujinga wa wenziye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…