Jamaa kanunua laini mpya ya simu akajitumia sms "mwambie mkeo aachane na mume wangu" kufika nyumbani akampa yule mwanamke ile sms asome mke akapaniki sana mara ooh majirani hao hawapendi kuona tunavyoishi kwa amani na upendo mara huyo atakuwa mama Kibandiko ndiye nimemchamba juzi, jamaa kimya. Kesho yake akapigiwa simu anahitajika kwa mjumbe kufika kule anamkuta mwanamke ana manundu kuuliza kuna nini akaambiwa yule mwanamke amepigwa kwa sababu ya kumtumia yeye sms, jamaa akabaki anashangaa.
Kumbe mke wake alikuwa na mchepuko mtaa wa pili aliivyoona ile sms akajua tayari mke wa jamaa kajua akamwambia mchepuko wake kwamba mke wake katuma sms kwa mmewe na bila jamaa kujua akashusha kipondo cha haja kwa mkewe kwanini amemtumia jamaa sms.
Ukweli ukawa umejulikana.