Inategemea mlivyozoeshana. Mi wife alikuwa na kawaida ya kuniagiza 'ukirudi naomba pitia dukani ninunulie skons za mtoto anywee chai akienda shule, niletee ubuyu nna hamu nao na vikolokolo vya jinsi hiyo, mwanzoni nilimkubaria lkn akataka kufanya mazoea nikamuuliza hivi wewe huyu housegirl na wewe mnashindwa kwenda dukani kuandaa vitu vya mtoto mpaka mi na ndevu zangu kila siku nikaulize ubuyu? Akadai samahani kama unakwazika tutaenda wenyewe, nikamwambia sitaki kusikia tena huu upuuzi.
Kwa hiyo jinsi utakavyomzoesha ataendelea usichokitaka kikemee mapema sana.