Hi imekaaje wadau

Hi imekaaje wadau

thehunk

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2011
Posts
533
Reaction score
233
WAFANYAKAZI wanne wa Benki ya Access Tawi la Manzese, jijini Dar es Salaam, jana walipandishwa kizimbani, kwa kosa la kuvunja baa na kuiba fedha taslimu Sh milioni 1.9. Wafanyakazi hao walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, wakidaiwa kuvunja na kuiba mali hizo zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 45, mali ya Rahmat Rashid Mandari.

Watuhumiwa hao ni pamoja na meneja wa tawi hilo, Fadhili Muzzo (32), Michael Milinga (28), Luca Timbuka (32) na Isaack Nchemba (33).

Wakisomewa shitaka hilo mbele ya Hakimu Anniseta Wambura, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Jackson Chidunda, alidai kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo Januari 29, mwaka huu, maeneo ya Manzese.

Alisema washitakiwa walivunja baa iitwayo Manzese Bar and Guest House, kisha kuchukua vitu mbalimbali wakati wakijua kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Chidunda alidai kuwa vitu vilivyoibwa ni pamoja na Mixer ya muziki, dekoda moja, kreti 63 za soda, katoni moja ya soda cane, katoni 63 za maji ya uhai, katoni 63 za maji ya Kilimanjaro, kreti 11 za bia ya Serengeti na maboksi mawili madogo ya bia ya Serengeti.

Vitu vingine ni friji mbili aina ya LG, viti na meza na vitu vingine vingi. Mwendesha mashitaka huyo alidai kwamba pamoja na kuiba mali hizo, waliamua kuharibu mali zilizokuwapo katika eneo hilo.

“Mliharibu mlango mmoja wa grili, mlango mmoja wa mbao, vitasa vya milango pamoja na vinginevyo,” alisema Chidunda.

Watuhumiwa wote kwa pamoja walikana kosa hilo na upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea. Hakimu Wambura alitangaza kuwa dhamana ipo wazi kwa watuhumiwa, huku kila mtuhumiwa akitakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho vya kazi.

Washitakiwa walifanikiwa kutimiza masharti ya dhamana na kuachiwa hadi Mei 28 mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.


mimi ninachohisi hapa ni huu utaratibu wa Access Bank kumwambia offisa wa bank akatafute wateja mitaan amfanyie assessment na akiona anafaa ampe mkopo na marejesho yakishindwa kufanywa na mkopaji basi offisa aliyempa huo mkopo yuko liable kwa kutakiwa kulipa sasa kupisha hiyo adha ofisa anaweza fanya any means necessary ili tu mkopo urudi ss matokeo yake ndo kama haya kuvunja vitu vya watu kuogopa kukosa kazi pamoja na kulipa pesa ya bank........Ndo mana mi nikisema vitu vingine vinavyoonekana kama opportunity si opporutinity bali ni kujiingiza matatizoni tu (ila ukisema hivyo unaonekana unachagua kazi) kwa hili la access huoni kwamba bank wanakukopesha mfanyakazi ili ukakopeshe hao wateja kwani wamekuwekea kiwango kwa mwezi lazima ukifikie hapo hapo malipo ya mkopo wewe ndo uko responisble akishindwa unawajibika sasa si kwa ujumla wewe ndo unamkopesha na wala si bank.....jamani inauuma sana hili poleni kwa nyie mliokutwa na hii kadhia
 
da! Hawa access bank nimeomba kazi kwao brach ya dar mpaka leo sijui zimeshia wapi.. Then ilikuwa ndo hiyo afisa mikopo.. Da! Kumbe ndo hivyo watu wanateseka
 
sidhani kama kuna kesi hapo, nahisi jamaa walienda kuchukua hivyo vitu kwa sababu mwenye mali anadaiwa mkopo wa bank. Nahisi walipofika mwenye mali akavifungia ndani ndipo jamaa walipovunja kitasa kwa nia ya kuchukua dhamana yao. If so, there is no case, wataachiwa tu at the end of the day!
 
Back
Top Bottom