Hezbollah: Lengo letu ni kuiangamiza Israel

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Hizbullah: Lengo letu ni kuuangamiza utawala wa kizayuni wa Israel
Apr 20, 2019 08:07 UTC
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, njia ya harakati hiyo ni kufuata maktaba ya Uislamu na kuuangamiza utawala ghasibu wa Israel unaoikalia kwa mabavu Beituul-Muqaddas.
Sheikh Naim Qassim amesema hayo mjini Beirut Lebanon katika mazungumzo yake na ujumbe wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kueleza kuwa, uhusiano wa Hizbullah na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni katika neema za Mwenyezi Mungu.
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amebainisha kuwa, misaada ya Iran hususan ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH kumeilea Hizbullah na kuipa nguvu na kuwafanya wapiganaji wa harakati hiyo wapate ushindi katika vita vyao na adui Mzayuni.
Amir Khojasteh, mkuu wa ujumbe wa Bunge la Iran naye amepongeza na kusifu mchango wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon katika kuunda mhimili wa muqawama na mapambano katika miaka ya hivi karibuni.
Katika kipindi cha siku mbili cha kuwa kwake Beirut, ujumbe wa Bunge la Iran unatarajiwa kukutana na baadhi ya viongozi wa makundi ya mapambano ya Kiislamu ya Palestina akiwemo Saleh al-Arouri, Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na Ziyad al-Nakhalah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina.
Tags
LEBANON
 
Hizbullah sio bongo army,anaweza akamteketeza muisrael na msiamini kilichotokea.
 
Hiyo ni ndoto ya mama yake na vifaranga juu ya Mwewe!
 
Ni wakati wa kumlinganisha Kimsboy na taifa analotukana kila siku:-
Eneo moja tu la Afya:

· Israel wameweza kubadili mimea jamii ya algae kuwa tissue za moyo (heart tissues), zinatumika kwenye upasuaji wa moyo

· Israel wamegundua kifaa kinachoitwa Sniffphone( a device that can smell diseases) kinaweza kugundua mgonjwa anaumwa nini hasa kwa anayeshindwa kujieleza vizuri kwa daktari ama mgonjwa mahtuti

· Wamegundua kamera inayoweza kumezwa na kusoma maendeleo yote ya mwili na taarifa kutumwa nje ya mwili; hiki chombo huweza kumeng’enywa (digestible) na enzymes za mwili na kutolewa kama uchafu (a swallowable medical camera)

· Wamegundua kitu inaitwa “a battery-packed ‘exoskeleton”. Ni mfano wa skeleton ya nje inayowezeshwa na betri kumsaidia mtu aliyepoteza miguu kwa ajali kutembea kama ana miguu ya kawaida

Kimsboy:
Nadhan hata uandishi wake usio na nukta, koma wala paragraph inatosha kusema Taifa lenye faida duniani litaishi milele na mtu ama kijikundi cha watu chenye mawazo hasi kitaangamia na kupotea
 
Back
Top Bottom