Hewa Yenye Sumu Yamkimbiza Meya Ofisini Jijini Mwanza

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,267
Meya wa jiji la Mwanza, James Bwire (CCM) amelazimika kukimbia ofisi yake baada ya mashine inayotumika kutoa hewa safi, (AC) ndani ya ofisi hiyo kutoa hewa inayosadikika kuwa na sumu.

Meya huyo amewaeleza waandishi wa habari kuwa tukio hilo limetokea ikiwa ni mara ya pili katika ofisi yake, ambapo awali alilazimika kulazwa katika hospital moja jijini Nairobi kutokana na kuvuta hewa kama hiyo ndani ya ofisi hiyo.

Hata hivyo jeshi la polisi limeanza uchunguzi kubaini dhidi ya madai ya kupuliziwa hewa ya sumu ofisini kwa mstahiki meya wa jiji hilo la Mwanza James Bwire,ambapo tayari limewahoji watu kadhaa kuhusiana na tukio hilo lililotokea juni 13 mwaka huu.

Madai ya sumu kupulizwa ofisini kwa Meya huyo, yaliibuka muda mfupi baada ya Meya huyo kuingia ofisini akitokea kwenye ziara ya kukagua maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo eneo la Sinai.

7ffb5fb4a1d7d9bc3a1da60d0d9c3955.jpg
 
Back
Top Bottom