HESLB yasitisha mikopo kwa maelfu ya wanafunzi

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesitisha kwa muda mikopo kwa wanafunzi 2,739 walioshindwa kujitokeza wakati wa kuhakiki wanufaika wa mikopo hiyo.

Aidha, imetoa siku saba kuanzia jana kwa wanafunzi ambao hawakuhakikiwa kwenda kuhakiki katika vyuo vyao, vinginevyo mikopo yao itafutwa na kutakiwa kurejesha kiasi walichokopeshwa na kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Jerry Sabi, alisema hatua hiyo imetokana na kuwatilia shaka wanafunzi walioshindwa kujitokeza kuhakikiwa.

“Tumesitisha mikopo kwa wasiohakikiwa kwa sababu hatujui kama ni wanafunzi halali au hewa. Tunataka kuwahakiki pia kwa kuwa hatujui kama wakati tunahakiki wengine walikuwa wagonjwa au wamerudia mwaka au wana sababu nyingine,”alisema.

Mei mwaka huu, Wizara ya Elimu, Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, aliagiza kufanyika uhakiki kwenye taasisi za elimu ya juu nchini kubaini kama kuna uwepo wa wanafunzi wasiostahili kupata mikopo.

Kuanzia Mei 30, mwaka huu, HESLB ilifanya uhakiki katika vyuo 26 na tayari imeshafanya uchambuzi wa uhakiki kwa vyuo 18 kati ya hivyo.

Akizungumzia uhakiki huo, Sabi alisema ulifanywa na timu maalumu iliyoundwa na Bodi kwa kuhakikiwa mwanafunzi husika na kubaini kuwa wanafunzi 2, 739 hawakujitokeza kuhakikiwa. Aliongeza kuwa, Uchambuzi katika vyuo vinane unaendelea.

Hata hivyo, bodi hiyo haikueleza ni wanafunzi wangapi walihakikiwa katika vyuo ambavyo kazi ya uhakiki imefanyika. Alisema bodi itafanya uhakiki wa awamu ya pili ili kujiridhisha kabla ya kuwatangaza kuwa ni wanafunzi hewa na fedha ambazo zitakuwa zimeokolewa kutokana na kuwabaini wanafunzi hao.

Alisema majina ya wanafunzi ambao hawakujitokeza kuhakikiwa wakati wa uhakiki vyuoni yamewekwa kwenye tovuti ya Bodi na pia katika vyuo ambavyo vitafanya utaratibu wa awamu ya pili ya uhakiki.

Alivitaja vyuo vilivyohakikiwa, kufanyiwa uchambuzi wa awali na idadi ya wanafunzi ambao hawakujitokeza kuhakikiwa kwenye mabano kuwa ni Chuo Kikuu cha Dodoma (763), Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha (126), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino- Mwanza( 232), Chuo Kikuu cha Mzumbe (66) na Chuo Kikuu cha Teofilo Kisaji-Mbeya (130).

Vingine ni Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino-Mbeya (21), Chuo cha Mtakatifu Yohane- Dodoma (262), Chuo Kikuu cha Mkwawa (103), Chuo Kikuu cha Iringa (100) na Chuo Kikuu cha Tiba-Bugando (43), Chuo Kikuu cha Arusha (55), Chuo Kikuu cha Jordan (128), Chuo Kikuu cha Makumira- Arusha (98), Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (385), Chuo cha Ufundi Arusha (22), Chuo Kikuu cha Waislamu-Morogoro (130), Chuo cha Uhasibu (57) na Chuo Kikuu cha Mount Meru (17).

Sabi alisema kutokana na kuwepo wanafunzi ambao hawajajitokeza, muda wa uhakiki umeongezwa hadi Agosti, mwaka huu.

Chanzo: Habarileo
 
Ninatumaini yanayofanyika kwa sasa yataleta matokeo chanya katika muhula mpya wa masomo.

Ikumbukwe kwenye kadhia za aina hii matokeo hupatikana baada ya kupitia njia tatu ambazo ni short term, medium term, and long term.

Short term huwavuruga watu mbali mbali, medium term hutuliza vurugu na kutoa mwelekeo na long term ni muda wa kupata faida.

Kelele mbali mbali zionazopigwa kwa sasa ni kwa sababu kuna watu wanavurugwa kwa njia mbali mbali.
 
Hakika wacha tuvurugane kwanza na tuvurugike ila mwisho tutakaa chini tukiwa tumeelewana. Hata wazungu ambao wana maendeleo walivurugana kwanza.
 
Hakika wacha tuvurugane kwanza na tuvurugike ila mwisho tutakaa chini tukiwa tumeelewana. Hata wazungu ambao wana maendeleo walivurugana kwanza.
Tanzania tulikuwa tunaelea kwenye fake economy bubble.

Bila kupiga stop mapema na kujiuliza tunaenda wapi, tungejikuta katika mazingira ya kuhatarisha usalama wa taifa au taifa kusambaratika.
 
Kama ni kweli watanzania tulikuwa tunahitaji mabadiliko basi ilikuwa ni lazima tupitishwe ktk kipindi kama hichi,maana nchi ilikuwa tayari imeshaoza sana.
Ngoja kwanza tuokwe tukitoka kwenye tanuru tutakuwa tumekaa sawa. Kila mtu alikuwa mpigaji. Watu walikuwa wanahonga wapate vyeo fulani wakapige. Nchi hii muda si mrefu ingegeuka kuwa nchi hewa.
 
Kama ni kweli watanzania tulikuwa tunahitaji mabadiliko basi ilikuwa ni lazima tupitishwe ktk kipindi kama hichi,maana nchi ilikuwa tayari imeshaoza sana.
Tulijisahau kama taifa na kwa sasa lazima tuifahamu misingi ya kazi halali au njia za kipato halali.
 
Eh kila kitu hewa inawezekana hata yale mafuta,gesi tulizoambiwa zimegunduliwa zikawa hewa....hebu tupitie hadi idadi ya wanyama walioko mbugani usikute tunajidai nchi yetu ni tajiri imebarikiwa na maliasili lukuki kumbe ni maliasili hewa...kwa mwendo huu hata kuwaamini wale waliotuletea matokeo ya uchaguzi inakuwa ngumu kuwaamini usikute huko nako kulikuwa na kura hewa:rolleyes:
 
Zoezi nzuri sana, uhakiki ufanyike pia kwa wanafunzi wanaosoma nje ya nchi kwani hata hewa bipo na wengine hela haiwafikie kabisa
 
Ngoja kwanza tuokwe tukitoka kwenye tanuru tutakuwa tumekaa sawa. Kila mtu alikuwa mpigaji. Watu walikuwa wanahonga wapate vyeo fulani wakapige. Nchi hii muda si mrefu ingegeuka kuwa nchi hewa.

Hoja hii iko general mno!Si sahihi kusema kila mtu alikuwa mpigaji,wapo Watanzania wengi tu waliolitumikia Taifa hili hadi tone la Mwisho ya jasho lao na wakabaki kuwa mafukara.

Upigaji ulikuwa dili la watu wachache lililokuwa linasimamiwa na kuratibiwa na vigogo wenyewe.Hakuna dili lolote ambalo mtu wa kawaida angeweza kupiga,madili yote yalikuwa na "koneksheni na wakubwa.Kila dili lililofanyika katika nchi yetu " ukikonekti doti",lazima utamkuta kigogo Mwenye mamlaka ya juu kahusika,mafano hai ni sakata la LUGUMI.

Sakata la LUGUMI ni moja ya dili linazoziunganisha familia za vigogo wa juu kabisa wa nchi yetu,kutokana na kuwahusisha watu wanene kabisa wa Taifa letu,ndiyo maana hata njia zinazotumiwa kulimaliza sakata hili zimekuwa za tahadhari kubwa sana ili kuwalinda vigogo wenye mkono wao katika sakata hili.
 
Ninatumaini yanayofanyika kwa sasa yataleta matokeo chanya katika muhula mpya wa masomo.

Ikumbukwe kwenye kadhia za aina hii matokeo hupatikana baada ya kupitia njia tatu ambazo ni short term, medium term, and long term.

Short term huwavuruga watu mbali mbali, medium term hutuliza vurugu na kutoa mwelekeo na long term ni muda wa kupata faida.

Kelele mbali mbali zionazopigwa kwa sasa ni kwa sababu kuna watu wanavurugwa kwa njia mbali mbali.
hahahaha umeua mkuu na hii kitu ni mbaya mnooooooo kuliko cha kushangaza ndo kimeingiliwa kabisa.
 
Back
Top Bottom