mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 14,192
- 19,118
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na TCU, majina ya wanafunzi watakaokuwa wamedahiliwa katika vyuo vikuu mbalimbali yatatoka rasmi tarehe 2/10/2017. Lakini vyuo vitafunguliwa tarehe 30/10/2017.
Hivyo bodi ya mikopo watakuwa na mwezi mzima wa kufanya zoezi la kuchakata upangaji wa mikopo kwa waombaji wa mikopo hiyo. Kitu ambacho hatutaki kusikia ni kuona mpaka vyuo vinafunguliwa na mikopo kwa waliopata kuwa bado haijawa tayari.
Tunataka mwanafunzi atakapofungua chuo, pesa zake za mkopo ziwe tayari zipo na akitoa akaunti yake tayari aweze kuingiziwa pesa zake. Wahusika wote washughulike sasa. Kama ni wizara ya fedha au hazina, basi waanze kujipanga sasa, siyo wasubiri kusukumwa na maandamano ya wanafunzi pale UDSM.
Hilo tumelichoka. Ambaye atakuwa amekosa mkopo, basi ajue mapema aamue kusuka au kunyoa mapema. Siyo kumwacha mtu amesharipoti chuoni na kisha kuambiwa hajapata mkopo. Au mtu anaambiwa amepata mkopo lakini anakaa zaidi ya mwezi mzima akiwa hajaingiziwa pesa zake kwenye akaunti. Tumetoa ilani mapema!