beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,881
- 6,377
Habari wadau, natumaini wote ni wazima wa afya.
Hadi kufikia sasa, ni wanafunzi wengi sana tayari wamekatishwa tamaa ya kusoma. Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) ni tegemezi pekee la walio wengi ili kuweza kumudu gharama za kujiunga na chuo.
Kumekuwa na sintofahamu kuhusu hatma ya wanafunzi wengi kwani hata wale ambao wana ufaulu mzuri na wamechaguliwa kujiunga na masomo ambayo hapo awali yalikuwa yanapewa kipaumbele wamekatwa na hadi sasa hawaelewi kinachoendelea.
Tatizo haswa ni nini? Upatikanaji wa mikopo umekuwa mgumu sana hata kwa wale ambao wanakidhi vigezo vyote. Wanafunzi wanaotoka kwenye familia zenye uchumi wa chini hawana tena matumaini. Licha ya ufaulu mzuri, wanakosa nafasi kisa tu hawana uwezo kifedha.
Hii inawaacha wapi watanzania hawa? Ina maana wanakosa haki yao ya msingi ya kupata elimu sababu tu hawana pesa? Serikali ina mpango gani na kundi hili? Malengo yao ndo yamezimika kabisa? Ni kwamba hakuna fedha za kutosha au taratibu za kupatiwa mkopo zimebana zaidi? Tunategemea wataalamu watatoka wapi ikiwa mambo yenyewe ndiyo kama haya?
Japokuwa kinachoendelea kinakatisha tamaa, bado wanafunzi wana nafasi ya kurekebisha taarifa zao na kukata rufaa kwenye bodi hiyo. Dirisha lipo wazi na huenda matokeo yakawa mazuri zaidi.