Heshimu pesa-usizipende

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,065
Reaction score
61,397
heshimu pesa-usizipende
Kwa mpishi,kisu chenye makali Ni kifaa muhimu.lakini kisu hicho hicho kinaweza kuleta madhara makubwa kikiwa mikononi mwa mtu asiye na ujuzi au asiye makini.PESA Ni kama kisu chenye makali.ukijua jinsi ya kuzitumia,zitakuwa na faida kwako.lakini usipokuwa mwangalifu,unaweza kuumia.mfano hata watu fulani wameazimia kuwa matajiri,na katika harakati hizo wamepoteza marafiki,wamevunja mahusiano ya kifamili,na mbaya zaidi kuharibu uhusiano wao na Mungu.kwa sababu hiyo "wamejichoma wenyewe kila mahali kwa maumivu mengi"..mwisho wa siku jifunze kutumia pesa inavyofaa.ziheshimu,lakini usizipende!nadhani mmenielewa vijana wenzangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nimekuelewa.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…