Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
OriginExpand
Middle English
Anglo-French
Middle French
Latin
Kumezoeleka katika mada, matangazo, taarifa, habari, uandishi, uchambuzi na kadhalika kuanza na President Dr. Kikwete, au Profesa President Dr Kikwete, ni makosa kitaaluma na maana halisi ya nafasi, maana, mazingira ya matumizi ya majina hayo ya heshima. Pengine ukimya wa Rais kutotoa mwongozo na kubaki kukubaliana na kuitwa hivyo dalili kwamba anapendelea hivyo lakini ukweli ni upotoshaji mkubwa wa maana, nafasi ya matumizi sahihi ya majina ya heshima.
Viongozi hawa wakitajwa moja kwa moja majina yao halisi bila majina ya utambulisho wa nafasi na majukumu yao hapo majina ya hashima hutangulizwa kabla ya jina lake kama Horn Kikwete, Dr Kiwete, Professor Kikwete nk.
President ni cheo na heshima ya juu zaidi katika nchi. Hakuna jina wala hadhi ya heshima zaidi ya kuwa mkuu au kiongozi wa nchi. Nilishaongelea mada hii huko nyuma lakini ni kukumbushia tu vinginevyo tunaonekana mbumbumbu kabisa, na hata Rais mwenyewe kukubali hivyo anaonekana kutokuwa makini, nakumbuka Nyerere alikataa katakata kutokana na uelewa wake na hakuna aliyethubutu kumwita hivyo.
Inaingia akilini
Wanasiasa wanaonekana elimu hii imewapiga kikumbo ndio maana utaona kama ifuatavyo
Mheshimiwa Mbunge, Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa makamu wa rais, mheshimiwa Katibu Mkuu, mheshimiwa mkuu wa wilaya. Wabunge ndio kabisa wamevimbishia mishipa kuitwa waheshimiwa. Mheshimiwa spika wa bunge, speaker ni heshima ya juu kabisa bungeni na hakuna zaidi yake, lakini imezoeleka hivyo, ila ni jambo linalohitajika kufanyiwa kazi.
Wanaopendelea na kufurahia kuitwa hivyo dhahiri hawajaelimika na tunahitaji kuwaelimisha. Ndio maana nyumbani baba ataitwa baba na mama ataitwa mama si mheshimiwa mama au mheshimiwa baba.

- Mufti wa kiislamu umwite Mheshiniwa Mufti?
- Cardinali umwite Mheshimiwa Kardinali?
- Shekhe umwinte mheshimiwa shekhe?
- Askofu umwite mheshimiwa Askofu?
- Imamu umwite mheshimiwa Imam?
- Padre umwite mheshimiwa Padre?