beevenom
JF-Expert Member
- May 1, 2017
- 313
- 433
Kwa namna ya kipekee kabisa kutoka ndani ya mtima wangu napenda kuwa moyo na kuwapongeza watumishi wa sekta ya afya kwa kazi nzuri mnayofanya. Tunajua kuna changamoto nyingi mnapitia lakini niwatie moyo kazi zenu ni zaidi ya kazi na niseme ni kazi ya Kimungu kabisa( ukifanya kazi hizi ni sawa na kufanya ibada kabisa).
Jamani wadau wengine tuna taaluma tofauti na wao lakini nimetafakari Sana sana ninyi mmeshikilia dhamana ya afya zetu,na mnafanya pasi kujali mnapokea nini. Ningekuwa kiongozi one day sekta hii inastahili kupata posho nzuri.
Nayasema haya leo nimempeleka mgonjwa aliyepata ajali kwa kweli alivyokuwa na huduma alivyopata hakika nimewapenda bure. Simaanishi kuwa fani nyingine hazina umuhimu ila hii ya afya ina upekee uliotukuka na niwaambie walimu kuwa kazi ya wito sio ualimu bali ni afya
Nawasilisha