Heshima kwenu wadada/wakina mama mlioolewa na kuishi ukweni hasa kwenye familia zenye watu wengi

Cheef Baroka

JF-Expert Member
Mar 24, 2020
330
1,000
Wana MMU mlio wengi mnapenda thread za kulana matunda kimasihara, kuchakatana yani Ngono na bata kwa ujumla. Leo naomba tujadili mambo yakifamilia zaidi hasa zile za kiswahili. niwakumbushe wale tulopita kwenye familia za mlundikano wa ndugu, je, tunawakumbuka wale wake za kaka zetu, na mama zetu wakambo tulokuwa tunaishi nao kwenye mfumo huu wa maisha usoisha, masengenyo, magomvi, umbea, majungu na wengine huingiza hadi imani za kishirikina?. Unamchukuliaje mdada huyu anaeolewa hapa anazaa watoto wake kadhaa au wote hapa, anaanza toka binti hadi mtu mzima katika maisha haya?. Hebu tuvute kumbu kumbu hata kama si kwetu hata kwa Jirani mambo yalikuaje?

Nakuheshim sana we dada unayeishi na mawifi zaidi ya wa3, mashemeji 7, Watoto wa mawifi na mashemeji (kama krinik), baba mkwe na MAMA mkwe, shangazi/ mjomba. Nikivuta hisia nikajaribu kuvaa uhalisia wako , Sina Maneno yakukwambia ila kama umeweza kuishi katika hali hiyo nahisi hata motoni hapatakupa tabu ( natania) UBARIKIWE KULIKO WANAWAKE WOTE DUNIANI.

Afu unakuta lijanaume limeshiba ugoro na bangi linalopoka tu "Wanawake wote ni M mbwa " . Mmbwa mwenyewe kenge wewe
 
Cheef Baroka

JF-Expert Member
Mar 24, 2020
330
1,000
Acha utoto Mimi nimekaa New Zealand Norway na italy familia niliiacha kwa mama yangu mzazi Tanzania na hakukuwa na shida.
Shida sio kuiacha familia nyumbani kaka, shida nyumbani mpo wangapi? Familia nayomaanisha apo ni zile za kiswahili mmerundikana kama msibani. Nahisi hujapitia huko
 
Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,031
2,000
Kumbe na wewe ni mwanamke ndio maana umeamua kujisifia hapa kiaina na kurudisha tusi la kuitwa mbwa, hongera mama itunze ndoa yako.
 
cocastic

JF-Expert Member
Nov 30, 2019
8,706
2,000
niliwahi geuza kurudi nyumbani kutoka kwa babu na bibi, yaaan nlikuta karibu nusu ya ukoo mzma uko hapo khaaaaah.
 
Espy

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
68,846
2,000
Siwezi olewa nikaishi ukweni aisee, huko pakusalimia siku mbili tatu na kusepa, ndoa ya wawili na sio ukoo.
Sasa kule uchagani unakuta watoto wote wa kiume wamepewa eneo hapo hapo nyumbani wajenge. Bora awe anaishi sehemu tofauti na nyumbani ni hadi wakati wa hija au mambo mengine. Ila ndio ukute wote wanaishi hapo basi ni shughuli mtindo mmoja.
 
cariha

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
13,440

Hahaaa Ila pale kila mtu huishi nyumba yake Ina uafadhali kuliko kuishi under one roof, pika tupakue hapo ndo shida, ugomvi hauishi. Mimi siwezi kabisa kwanza huwa mkimya na Mambo ya kupangiwa siwezi na sipendi mazoea kabisa sijui mwali hiki mwali kile
 
mrsleo

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
2,491

we una tabia kama zangu
 
cariha

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
13,440
2,000
we una tabia kama zangu
Maandiko yenyewe yanasema utaacha baba na mama yako mkaanzisha mji wenu, mkikaa pamoja ugomvi haukwepeki mama mkwe mwenyewe atakuwa anaona unafaidi kwa mwanawe au una mloga vile mwanawe hampi attention hapo Sasa inaanza Vita na hivi wanaume wakioa husahau mama zao, na wamama hupenda watoto wao wa kiume, hapo lazima tu kuwe na vita
 
mrsleo

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
2,491
2,000
Japo sijawahi kuishi maisha hayo, ila nna shangazi yangu kwake pako hivyo yani yule kwake ndo kama makimbilio ya wooote walioshindwa maisha au pakuanzia, mtu kashindwana na mume anabeba watoto anahamia pale, sijui mtoto wa baba mdogo/shangazi imekuaje anaenda pale, wadogo zake (mana yy ndo mkubwa) ambao bado hawajatoka kimaisha wako hapo, mtu kaoa huko maisha yamekuwa maguma anabeba mke na watoto anaenda pale yaani mmh ile nyumba nishuguli pevu, wengine ndugu wa mbali na wenyewe wapo. Ofcoz amejaliwa kipato kidogo, na ana nyumba kubwa na hana mume wala mtoto
 
Ulweso

JF-Expert Member
May 24, 2016
15,851
2,000
Sasa kama mme hawezi kuoa nakujitegemea wakazi gani, mie siwezi ila wao huwa wanajuana kabisa wanapo oana, maana mwanamke anajua kabisa hili nibogasi halina uwezo wakupanga chumba tutaishi hapo hapo, nawapa hongera hao wanawake mie hapana siwezi
 
mrsleo

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
2,491
2,000
Maandiko yenyewe yanasema utaacha baba na mama yako mkaanzisha mji wenu, mkikaa pamoja ugomvi haukwepeki mama mkwe mwenyewe atakuwa anaona unafaidi kwa mwanawe au una mloga vile mwanawe hampi attention hapo Sasa inaanza Vita na hivi wanaume wakioa husahau mama zao, na wamama hupenda watoto wao wa kiume, hapo lazima tu kuwe na vita
hakuna kitu kigumu kwa ndoa kama kwenda kuishi na wakwe hata wakisema wanawapa kiwanja kwa pembeni ya nyumba yao mjenga still sio maisha utaishi kwa stress maisha yako yote
 
Ulweso

JF-Expert Member
May 24, 2016
15,851
2,000
Hahaaa Ila pale kila mtu huishi nyumba yake Ina uafadhali kuliko kuishi under one roof, pika tupakue hapo ndo shida, ugomvi hauishi. Mimi siwezi kabisa kwanza huwa mkimya na Mambo ya kupangiwa siwezi na sipendi mazoea kabisa sijui mwali hiki mwali kile
Mie mwenyewe siwezi, unaolewa na mwanaume badala mfurahie maisha ya ndoa mnakuwa kama mpo shule vile halafu wewe ndiyo mpishi hakuna kupumzika majungu umbeya, mmm kuongea ongea mie hata siwezi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom