Heshima kwa waalimu wa chekechea & class one | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Heshima kwa waalimu wa chekechea & class one

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Shoo Gap, Sep 7, 2012.

 1. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kuna mambo mengi kwenye maisha ya kujivunia, ktk elimu leo ninapenda kumkumbuka Mwalimu wangu wa chekekea aliyenifundisha kusoma na kuandika. Hawa waalimu huwa wanafanya kazi kubwa sana sana ambayo inathaminiwa kidogo sana na jamii. Ebu fikiria ni mambo mangapi umefaidi kwa kujua tu kusoma na kuandika? Ilipotokea kijana kafika F1 bila kujua kuandika na kusoma tunabaki kujiuliza maswali mengi tu, Inakuwaje? Ila watu hawafikiri inakuwaje huyu Mwalimu wa chekekea anaweza kuwasaidia hawa watoto wa miaka 5 hadi 8 kuweza kuandika na kusoma na kuelewa maana ya kile wanachokisoma.

  Mwalimu huyu zaidi ya kusoma na kuandika alinifundisha namna ya kupika chai, uji, kunawa uso, kuswaki, kufua, kupasi nguo n.k. Nakumbuka enzi hizo nukiwa na visoda vyangu shingoni ninawahi shule, darasani kulikuwa na vibao ambavyo tulijifunzia kuandika kwa kutumia chaki, wakati mwingine tuliandika chini wenye vumbi n.k. Tulijifunza michezo mingi mbalimbali, nyimbo zenye maudhui na mafundisho mbalimbali.

  HUYU MWALIMU KAJENGA MSINGI MUHIMU SANA MAISHANI MWANGU.

  Binafsi niko ktk mchakato wa kutafuta zawadi ya kumuenzi Mwalimu wangu huyu, niombe wasomi wenzangu kuwakumbuka watu kama hawa waliojenga msingi ktk maisha yetu ya elimu.

  Haya nimeona baada ya kuona wanangu wanavyopiga hatua kiakili wakiwa na waalimu wao hawa.
   
 2. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Nashukuru Mungu kwa kukupa utambuzi na busara hadi ukaamua kumshukuru/kuwashukuru walimu tajwa hapo juu!!!
  Hamna kazi kubwa kama kufundisha watoto wadogo wa nursery au darasa la kwanza kwani inabidi hata mwalimu awe mpenda watoto pia awe ana act km mtoto ili aweze kumfundisha/kuwafundisha na waelewe jinsi ya kuandika au kusoma.

  Nakumbuka wimbo wa "Hii ndiyo "a" ina mkia mfupi a a a a......
   
Loading...