Heshima kitu cha bure! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Heshima kitu cha bure!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jpinduzi, Dec 14, 2011.

 1. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kamusi ya “Oxford inatafsiri “Kujiheshimu” kama “mawazo” mazuri kuhusu tabia ya mtu mwenyewe” Iwapo unajiheshimu sana, maana yake ni kwamba unajisikia vizuri.Unajua kwamba unayothamani - mtu unayestahili kupendwa. Unajiheshimu mwenyewe.

  Hisia za namna hii ni nzuri sana, unapojihisi kupendwa na kuheshimiwa unategemea hivyo hivyo kutoka kwa watu wengine vilevile.
  Unapojiheshimu sana haina maana ya kwamba wewe huwezi kujichukia au kujikasirikia mwenyewe. Kuna wakati kila mtu hukata tamaa, lakini yule mwenye kujiheshimu anakubali makosa na kusonga mbele.Kujiheshimu ni tofauti na kujidai au kuwa na majivuno mengi.Watu wanaojienzi wanajipenda, lakini haina maana ya kwamba wanajifikiria wao hawana dosari yoyote, au wao ni bora kuliko wengine.

  • Fikiria wewe ni mtu wa aina gani na kutengeneza orodha ya sifa ulizonazo. Unapenda nini kuhusu wewe mwenyewe? Wema wako? Ucheshi? Ubunifu? Umakini?

  • Fahamu mambo yanayokuhusu ambayo ungependa kuyaboresha, lakini usijikosoe sana.

  • Kuwa mhalisi na weka malengo ambayo yanatekelezeka na yatakayoonyesha mafanikio ili uridhike unapoyakamilisha.

  • Jiamini, na jiambie “ninaweza!”.

  • Tumia muda wako na watu wanaokujali wanaofanya ujisikie vizuri na kuongeza hadhi ya kujiheshimu. Kaa mbali na watu wanaojaribu kuharibu heshima yako, hasa kama wanafanya hivyo kwa sababu fulani.Kwa vyovyote vile kuifanyia kazi heshima yako haina maana kuwa hutaweza kupata matatizo.Kuifanyia kazi heshima yako itakusaidia matatizo kuwa mepesi. Kujiheshimu kunakulinda wewe binafsi.

  Wakati mtu anakutendea vibaya hisia za kujiheshimu zinapiga kelele “Hee! haya ni makosa, usiruhusu mtu huyu akakutendea hivi”.Hebu fikiria kana kwamba marafiki zako wamekuacha. Wamejiunga pamoja na kukuacha peke yako. Ghafla unajisikia kutetemeka na huna uhakika wa mambo yako. Ni kwa nini hawakutaki tena? Je kuna makosa umefanya? Heshima yako inaanza kufifia kama ua linavyonyauka.Unaanza kujisikia vibaya.

  Katika mazingira ya namna hii, watu wengine hupata hofu. Wanachukua njia rahisi ya kurudisha heshima inayoshuka ili apendwe tena, hata kama itamaanisha kufanya jambo ambalo wanafikiria ni kosa. Kwa mfano, vijana wengine ambao wamekataliwa na marafiki zao wa zamani huanza kujiunga na makundi ya vijana wanaokunywa pombe, wanaovuta bangi na kujiingiza kwenye matatizo makubwa. Hivyo wanaanza nao kula madawa ya kulevya, kunywa pombe ili waweze kukubalika.

  Ni vizuri kutafuta kukubalika na kweli inapandisha hadhi lakini haisaidii kutatua matatizo ya kujiheshimu na wala kukubalika hakudumu. Unaweza kujisikia vizuri kwa muda lakini baada ya muda mfupi sauti ndogo ndani yako huanza kukusumbua: “Watu hawa hawako makini”. Sauti hii ni kwamba haujawa mkweli kwako mwenyewe, unajizuia kufanya mambo unayoyataka na unayoyaweza. Hujisikii vizuri kutokana na yale unayoyafanya kwa mkumbo...” Hiyo sauti ndogo ni nafsi yako.

  Ni vema wakati wowote kuisikiliza.Kurekebisha kujienzi kwako ni kazi kubwa kuliko kujiunga na makundi mapya, au kupoteza mawazo kwa kutumia pombe, na madawa ya kulevya. Itakusaidia zaidi kurekebisha kujienzi kwako. Unapopitia matatizo ya kujienzi, yafuatayo ni mambo machache unayoweza kuyafanya ili yakusaidie:-

  • Jaribu kuliweka tatizo lililopo katika mtazamo sahihi. Jaribu kukumbuka kwamba dunia imejaa mambo ya raha na shida, na kwamba huu sio mwisho wa dunia.

  • Zungumza na mtu wa karibu yako na unayemwamini kuhusu matatizo yako na hisia zako. Mtafute kijana mtoa ushauri nasaha au mtu ambaye anakujali na ambaye anaweza kukusaidia.

  • Kumbuka kuwa watu wengine wanakuthamini kutokana na vile ulivyo. Mtafute mtu ambaye atakuthamini – rafiki mpya, dada, kaka, mzazi au ndugu mwingine.
  • Kuwa mvumilivu. Kujiheshimu hakujengeki katika siku moja.Unaweza kujisikia vizuri baada ya siku kadhaa
   
 2. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Mantik ! Mtiririko umeutiririsha vizuri ! Bt sorry are you politician?
   
 3. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Thanks,am not a politician.
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Mada nzuri sana. Ukijiheshimu unajua jinsi ya kugombana na kusimamia unachokiamini kwa heshima. Tungejiheshimu wote humu maybe kusingekuwa na haja ya ban na paw angekosa kazi!
   
Loading...