Kuandaa HESABU za KAMPUNI hasahasa kwa LTD ni muhimu sana kwa ustawi wa biashara yako na pia inatakiwa kisheria za Kodi na zaidi sana BRELA.
TENA kuandaa HESABU ZA KAMPUNI kutakusaidia kupanga mipango ya baadae ya biashara yako. Ukiwa na kumbukumbu za fedha utaweza kufanya maamuzi bora ya biashara yako hususani kuhusu vyanzo vya mapato, kodi, matumizi binafsi ya mmiliki wa biashara na hata kustaafu katika biashara.
AMA MJASILIAMALI au ni MFANYABIASHARA ni vyema sana uweke utaratibu wa kutunza taarifa sahihi za miamala ya kifedha inayofanyika na kuonesha namna fedha zilivyotumika. Utunzaji wa kumbukumbu za kifedha utakusaidia kutoa taarifa kuhusu namna taasisi inavyoendeshwa na ikiwa inafanikiwa kutimiza malengo yake ama la.
Umuhimu wa kumbukumbu
i) Taarifa: Kila biashara inahitaji kuandaa na kutunza kumbukumbu za miamala yake ya kifedha ili waweze kupata taarifa kuhusu hali yao kifedha, ikiwa ni pamoja na:
Taarifa fupi ya mapato na matumizi na mgawanyiko wake katika vipengele mbalimbali.
Matokeo ya shughuli za biashara – ziada (faida) au upungufu (hasara).
Mali na madeni – au vitu vinavyomilikiwa na biashara na vile ambavyo biashara inadaiwa.
ii) Uaminifu: Kutunza kumbukumbu sahihi za kifedha kunachochea uadilifu, uwajibikaji na uwazi, na kuepuka hisia za kukosa uaminifu hasa kwa wakopeshaji au wawekezaji ambao wangependa kushirikiana nawe katika biashara.
iii) Mipango ya baadaye: Pamoja na kuwa taarifa za kifesha zinaripoti mambo yaliyokwishatendeka, zinasaidia utawala kuweka mipango ya mbeleni na kuelewa zaidi kuhusu uendeshaji wa biashara. Ukiwa na taarifa za miaka miwili mitatu ni rahisi kupata taswira ya mwenendo wa biashara.
Namna za kutunza kumbukumbu za kifedha
Kumbukumbu za kifedha zinaweza KUANDALIWA kwa mfumo wa kuandika kwa mikono au kutumia mfumo wa kompyuta ambapo unaweza kutumia mojawapo ya programu za kihasibu za kompyuta.
Namba mbili kuu za utunzaji wa kumbukumbu za fedha ni:
Kurekodi kwa kuzingatia miamala ya fedha taslimu tu
Kurekodi kwa kuzingatia msingi wa muamala, hata ikiwa ni deni.
Itaendelea.
Kwa msaada wa KUANDAA HESABU ZA KAMPUNI/ ANNUAL REPORT/ANNUAL RETURN
- KUSAJILI KAMPUNI (LTD)
- BUSINESS NAME (JINA LA BIASHARA)
- PARTERSHIP (UBIA)
USAFI WA MAOFISINI, VIWANDANI, HOSIPITALINI, MASHULENI NK
Wasiliana nami kwa # 0 7 8 8 1 0 4 2 2 8 (SIMU / WATSUP)
Ushauri - Bure!